Amiri Jeshi Mkuu Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mkuu wa majeshi wa kwanza
Mzalendo Jenerali Mirisho Sarakikya muda mfupi baada ya kuwasili katika
chuo cha jeshi Monduli tayari kwa kutunuku kamisheni kwa maofisa 179
wapya wa jeshi waliohitimu vyema mafunzo yao mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na
usalama Jenerali Davis Mwamunyange kushoto na Mkuu wa Chuo cha Jeshi
(TMA) Monduli Brigedia Jenerali Paul Peter Massao(kulia) wakimsindikiza
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho kwenda uwanja wa Paredi ambapo
alitunuku kamisheni kwa maofisa wapya wa jeshi katika sherehe
zilizofanyika katika chuo cha jeshi(TMA) mkoani Arusha.
Mkuu wa Chuo Cha Jeshi Monduli TMA
Brigedia Jenerali Paul Peter Massao akimsindikiza Amiri Jeshi Mkuu Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kuingia katika viwanja vya Paredi chuoni hapo
akiwa katika gari maalumu ambapo alitunuku kamisheni kwa maofisa wapya
wa Jeshi.
Mkuu wa Chuo Cha Jeshi Monduli TMA
Brigedia Jenerali Paul Peter Massao akimsindikiza Amiri Jeshi Mkuu Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kuingia katika viwanja vya Paredi chuoni hapo
akiwa katika gari maalumu ambapo alitunuku kamisheni kwa maofisa wapya
wa Jeshi.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya
Mrisho Kikwete akipokea salamu ya heshima mara baada ya kuwasili katika
uwanja wa Paredi kutunuku kamisheni katika chuo cha jeshi Monduli mkoani
Arusha Jumamosi.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya
Mrisho Kikwete akikagua vikosi hkwenye uwanja wa Paredi la kutunuku
kamisheni katika chuo cha jeshi Monduli mkoani Arusha Jumamosi.
Maofisa Wapya wa jeshi wakipita
mbele ya mgeni Rasmi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na kutoa heshima
wakati wa gwaride maalumu la Kamisheni lilofanyika katika chuo cha TMA
Monduli.
Kikosi cha Bendera kikipita mbele
ya Amiri jeshi mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa gwaride
maalumu la Kamisheni lilofanyika katika chuo cha TMA Monduli.
Maofisa Wapya wa jeshi wakipita
mbele ya mgeni Rasmi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete nakutoa heshima
wakati wa gwaride maalumu la Kamisheni lilofanyika katika chuo cha TMA
Monduli.
No comments:
Post a Comment