Baadhi
ya wanahabari wakifuatilia kwa makini mafunzo kuhusu uandaaji wa wazo
na kuandika mpango kazi kwa ajili ya kuomba ruzuku kutoka mfuko wa TMFWanahabari nchini wametakiwa kutumia
fursa ya kuwepo kwa Mfuko wa kuwawezesha wanahabari wa TMF kutafiti na
kuandika habari zitakazoibua uchunguzi utakaosaidia jamii.
Wakizungumza wakati wa semina ya siku
moja iliyoandaliwa na Mfuko wa Vyombo vya Habari TMF kwa baadhi ya
wanahabari wa mkoa wa Mbeya, waandishi nguli wa tasnina hiyo Edda Sanga
na Ndimara Tegambwage waliwataka wanahabari kutumia vyema taaluma yao
kuibua,kuandika na kufanyia utafiti habari za uchuguzi ambazo zitaongeza
chachu ya maendeleo katika jamii.
Kwa upande wake Tegambwage alisema
kuwa wanahabari wengi wamekuwa wakiripoti habari za mijini ambazo
hazigusi uhalisi wa maisha ya wananchi wenye matatizo hivyo wanayo fursa
ya kuandika habari kwa undani wakilenga kuibua na hatimaye kufanyia
uchunguzi mambo yanayosababisha kero miongoni mwa jamii.
Alisema kuwa mwandishi anayejikita
katika habari za uchunguzi anapaswa kufanya utafiti wa awali utakaolenga
kuinufaisha jamii na kuangalia maslahi itokanayo na uchunguzi
atakaoufanya.
''Unachotaka kuchunguza kiangalie
kimelenga nini, kina uzito gani katika habari na pia uangalie upya wake
katika habari,''alisema Tegambwage.
Aidha alisema kuwa katika jamii
kumekuwa na matukio mengi yanayoibuka na kuelezwa kuwa yanatokana na
imani zinazoitwa kuwa ni za Ushirikina na kuwa mwanahabari anapaswa
kuandika hali halisi inayosababisha jambo linaloelezewa kuwa
linahusishwa na imani za ushirikina bila kuutaja ushirikina wenyewe.
''Ni ngumu tafsiri yake neno Ushirikina, elezea uhalisia wa tukio lenyewe kulingana na stori ilivyo,'' alifafanua.
Naye Edda Sanga aliwakumbusha
wanahabari kuandika habari kufanya bidii ya kujisomea badala ya kudhani
kuwa taaluma hiyo inaweza kufanywa bila kufuata maadili yake.
Alisema lipo kundi la watu
waliojiingiza katika taaluma ya habari na kufanya mambo ya habari bila
kufuata maadili na kusababisha upotofu wa maadili ya taaluma hiyo hivyo
ni vyema kila mwandishi akajitahidi kusoma na kujua miiko ya habari ili
kutopotosha umma.
''Kwa sisi tuliokuwa tukitangaza
zamani, tunaposikiliza matangazo ya kwenye Redio nyingi za sasa, kwa
kweli Wana ' boa' hawataki kwenda na changamoto zilizopo,''alisema.
Kadhalika aliwataka wanahabari
kufuatilia kwa kina uozo unaotendeka kwa baadhi ya viongozi wa umma
ambao kimsingi walipaswa kuwa ni kioo kwa wananchi.
Wakati huo huo aliyekuwa Ofisa Ruzuku
wa TMF Japhet Sanga ameaga rasmi kulitumikia shirika hilo alilodumu
nalo tangu mwaka 2010 na nafasi yake inachukuliwa na Dastan Kamanzi.
Akizungumza juu ya kuachia nafasi
hiyo Sanga alisema kuwa pamoja na kuwa amemaliza muda wake wa
kulitumikia Shirika hilo ataendelea kuwa karibu na wanahabari kwa
ushauri na mambo mbalimbali yahusuyo maendeleo ya taaluma hiyo na
maendeleo kwa waandishi wa habari.
Alisema wanahabari wamekuwa wakipata
changamoto nyingi katika utendaji wao na kuwa kuwepo kwa Mfuko wa TMF
umesaidia kuizindua serikali katika mambo mengi ambayo ilikuwa
imejisahau hivyo ni fursa kwa wanahabari kuutumia vyema mfuko huo kwa
kuibua kero zitakazowakumbusha watendaji kuitumikia jamii. | |
No comments:
Post a Comment