Mwenyekiti
wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akiongea na waandishi wa
Habari huku akiwaasa kuacha chuki katika masuala yanayohusu mchakato wa
Katiba
Mjumbe
wa Kamati Namba Nne ya Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Christopher Ole
Sendeka akiongea na wandishi wa Habari kuhusu kazi na majukumu ya Kamati
yake leo 28 Agosti, 2014
Mjumbe
wa Kamati Namba Tatu ya Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Dkt. Francis
Michael akiongea na wandishi wa Habari kuhusu kazi na majukumu ya Kamati
yake leo 28 Agosti, 2014.
Mjumbe
wa Kamati Namba Kumi na Moja, Mhe. Hamad Massauni akiongea na wandishi
wa Habari kuhusu kazi na majukumu ya Kamati yake leo 28 Agosti, 2014.
(Picha zote na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma)
Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma.
28/08/2014
MWENYEKITI wa Bunge Maalum la
Katiba, Mhe. Samuel Sitta amevitaka vyombo vya habari nchini kuacha
uchochezi na chuki wakati vinapohabarisha umma kuhusiana na mchakato wa
Katiba Mpya.
Kauli hiyo nimetolewa leo na Mhe.
Sitta wakati alipokutana na baadhi ya waandishi wa habari katika viwanja
vya Bunge mjini Dodoma huku akiviasa vyombo vya habari kuachana na
kuandika habari zenye kuleta uchochezi na chuki ili kuvuruga mchakato wa
Katiba Mpya .
Mhe. Sitta amesema kuwa kuna
baadhi ya watu wamekuwa na dhana tofauti kuhusu kazi ifanywayo na Bunge
Maalum la Katiba, hivyo ni vema kuepukana nao na kuhabarisha umma
taarifa sahihi ili Katiba Mpya iweze kupatikana.
”Kusema tunafanya kazi ya Tume ni
upotoshaji mkubwa, sisi tunafanya kazi tuliyotumwa tena kwa uadilifu
mkubwa.upotoshwaji mwingine unafanywa na baadhi ya watu ambao
hawalitakii mema Taifa letu na hawapendi kuona mchakato wa Bunge la
Katiba unaendelea vizuri,” alisema Mhe. Sitta.
Mhe. Sitta ameongeza kwa kutolea
ufafanuzi juu ya baadhi ya makundi yaliyowasilisha mapendekezo yao
katika Bunge hilo, kwa kusema kuwa maoni yanayoletwa na makundi
mbalimbali kwa lengo la kuboresha Rasimu Mpya ya Katiba yanapokelewa
lakini sio maoni tu ya mtu binafsi au mwananchi, bali wanapokea maoni
kupitia makundi maalum kama yalivyo kwa wafugaji, Wasanii na Wakulima
ambao wameshawahi kuwasilisha maoni na mapendekezo yao katika iliyokuwa
Tume ya Mabadiliko ya Katiba lakini hayakuonekana na mengine
yalisahaulika katika Rasimu hiyo.
“Tuna haki na wajibu wa kuyapokea makundi haya ili kutoa Katiba iliyo rafiki kwa wananchi wote,” alisisitiza Mhe. Sitta.
Wakati huohuo, baadhi ya Wenyeviti
wa Kamati mbalimbali za Bunge hilo, wamesema wamemaliza kazi ya
kuchambua Rasimu hiyo vizuri katika Kamati zao.
Akizungumzia kuhusu kazi hiyo,
Mwenyekiti wa Kamati Namba Tatu ya Bunge hilo, Dkt. Francis Michael
amesema suala la ardhi lilionekana kuwa nyeti katika Kamati yake.
Dkt. Francis aliongeza kuwa suala
la kupokea mapendekezo kutoka kwa makundi mbalimbali si kwamba kila kitu
kitawekwa kwenye Katiba Mpya bali ni yale mambo ya msingi.
Naye Mwenyekiti wa Kamati Namba
Moja ya Bunge hilo, Mhe. Ummy Mwalimu Ally na Makamu Mwenyekiti wa
Kamati Namba Kumi na Moja, Mhe. Hamad Massauni walisema kuwa katika
Kamati zao majadiliano yalikwenda vizuri.
No comments:
Post a Comment