Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Gabriel Kipija, akizungumza na Mbeya
yetu kuhusu mikakati ya kuongeza ufaulu kwa Wilaya hiyo.
Wanafunzi wakiwa Darasani
Mmoja wa wanafunzi Livingstone Msusi akielezea jambo kuhusiana na mkakati huo
Mmoja wa wanafunzi Salome Mwaiposa akielezea jambo kuhusiana na mkakati wa ufauru ulioanzishwa na Wilaya ya Kyela
Wanafunzi wakiwa Darasani
Hawa ni Baadhi ya wanafunzi watoro wakiwa wamekamatwa hapa wakipandishwa katika Gari
Huyu
ni moja ya wanafunzi watoro, hapa alikuwa amekamatwa amevaa nguo Tano
ndani kukwepa viboko, na katika picha hii anaonekana ameshikiria nguo
tatu ambazo anazionesha baada ya kuzivua huku zengine akiwa bado amevaa
Wanafunzi hao wakiwa tayari katika Gari hilo
Wanafunzi wakisikiliza Mkutano
Wanafunzi wakiwa katika Kituo cha Polisi Kyela
KATIKA kuhakikisha elimu inapewa kipaumbele na
kuongeza ufaulu kwa Wanafunzi Wilaya ya
Kyela mkoani Mbeya,Halmashauri hiyo imeanzisha mkakati maalumu wa kuwakamata
watoto wote watoro.
Hayo
yamebainishwa juzi na Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Gabriel Kipija, alipokuwa akizungumza kuhusu mikakati ya kuongeza ufaulu kwa wanafunzi Wilaya Kyela
Kipija alisema hali ya utoro kwa wanafunzi
ilikithiri sana kwa kutohudhuria masomo na kuzurura ovyo mitaani jambo
lililopelekea Halmashauri hiyo kushika nafasi ya mwisho kimkoa katika matokeo
ya hivi karibuni ya kidato cha Nne.
Alisema katika Operesheni iliyofanyika wiki
mbili zilizopita ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Magreth Malenga, yeye mwenyewe na Mkurugenzi wa
Halmashauri walifanikiwa kuwakamata wanafunzi 500 wa shule za Sekondari ndani
ya siku moja.
Alisema katika siku hiyo Wanafunzi wa shule
mbali mbali za Sekondari Kyela Mjini walikamatwa kwa uzururaji wengi wao wakiwa
kwenye sare za shule lakini hawakuhudhuria masomo na kuwafikisha kituo cha
polisi kwa kosa la utovu wa nidhamu.
Alisema kitendo cha kuwafikisha polisi wanafunzi
hao kimeibua mwamko mkubwa wa wanafunzi kuhudhuria masomo darasani pamoja na
kuwahi ambapo hivi sasa hakuna mwanafunzi anayeonekana barabarani kuanzia saa
moja asubuhi tofauti na awali.
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Keifo
iliyopo Wilayani Kyela ambao walikumbwa na mkasa huo, mbali na kukiri kufanya
vitendo hivyo tofauti na matarajio ya wazazi pia walipongeza kitendo cha
Halmashauri cha kuwakamata na kuwapeleka Polisi.
Livingstone Msusi(15) mwanafunzi wa kidato cha
Kwanza Keifo Sekondari alisema yeye binafsi alikumbwa na kamata kamata hiyo
lakini hivi sasa amejirekebisha na kuwa wa kwanza kuwahi shule tofauti na awali
ambapo alikuwa hafiki kabisa.
Salome Mwaiposa(14) alisema tangu operesheni
hiyo ifanyike amekuwa na maendeleo mazuri darasani kutokana na kuhudhuria
vipindi vyote na kwa wakati unaostahili.
Aidha baadhi ya wanafunzi waliwatupia lawama
wazazi kwa kutofuatilia maendeleo ya watoto wao mashuleni ikiwa ni pamoja na
kuwahimiza kwenda shule jambo lililochangia kuongezeka kwa utoro na kujiingiza
katika shughuli hatarishi mitaani.
Walisema ili kukomesha kabisa utoro wa wanafunzi
mashuleni ni bora wazazi wakatoa ushirikiaono kwa Serikali kwa kutoa taarifa
endapo wanakuwa na watoto ambao husumbua kusoma na kuwaletea kesi wazazi
kutokana na kujiingiza katika magenge ya uhalifu.
Na Mbeya Yetu
No comments:
Post a Comment