Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Serikali
imeagiza watumishi wote wa umma walipwe mishahara moja kwa moja kupitia
akaunti zao sahihi za benki ambazo zitatumika kupitishia mihahara yao.
Kauli
hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba alipokuwa
akiongea na waandishi wa habari ofisi za Hazina leo jijini Dar es
salaam.
"Mishahara
ya Watumishi wote wa Serikali, wakala na taasisi za umma italipwa moja
kwa moja kupitia akaunti zao za banki" alisema Mwigulu.
Ili
kufanikisha adhima hiyo ya Serikali, Mwigulu aliwaagiza waajiri wote wa
sekta ya umma kuwa wawe na akaunti namba za benki za watumishi wao wote
waliochini ya fungu husika ambazo zina taarifa sahihi na wakizingatia
mfumo sahihi wa taarifa za kiutumishi.
Mwigulu
alionya kuwa mtumishi asiye na akaunti benki asilipwe mshahara wake
dirishani ambapo amewahimiza waajiri kuwasisitiza watumishi walio chini
yao kufungua akaunti sahihi ya benki kwenye mfumo ambayo itatumika
kulipa mshahara husika kupitia orodha ya malipo ya mshahara (payroll)
inayotolewa na Hazina.
Aidha,
Mwigulu amasema kuwa kila ifikapo tarehe 10 ya kila mwezi waajiri wote
wawe wamewasilisha maombi ya fedha za kulipa mishahara kwa mwezi
unaohusika wakiambatisha orodha ya malipo ya watumishi ya kuthibitisha
kiasi kinachoombwa.
"Waajiri
watakaoshindwa kutoa 'Payroll' watasababisha watumishi wanaowaongoza
kushindwa kupata mishahara yao kwa mwezi husika jambo ambalo sio nia ya
Serikali" alisisitiza Mwigulu.
Utaratibu
huu wa kulipa mishahara utakuwa endelevu na umedhihirisha kuwa na tija
kwa matumizi ya fedha za umma kwani umeonesha mafanikio ambayo kwa mwezi
wa saba na wa nane hakuna mtumishi, Wakala za Serikali wala Taasisi
iliyolalamika kukosa mishahara.
No comments:
Post a Comment