Thursday, September 18, 2014

UMOJA WA VIJANA WAZALENDO WA VYUO VYA ELIMU YA JUU DAR ES SALAAM WATOA TAMKO LA KULAANI KAULI ZA MWENYEKITI WA CHADEMA TAIFA KWA MADAI YA KUHAMASISHA MAANDAMANO

 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Wazalendo wa Vyuo vya Elimu ya Juu Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Omary, akisoma tamko hilo, Dar es Salaam leo.
  Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Wazalendo wa Vyuo vya Elimu ya Juu Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Omary (katikati), akizungumza na waandishi wa habari wakati akisoma tamko hilo. Kulia ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Theodora Malata na Mwanachuo Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Rehema Akukweti.
Wawakilishi wa wanafunzi wa vyuo vikuu 12 vya Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Mwanachuo wa UDSM, Gulatone Masiga akijibu maswali ya waandishi wa habari. Kushoto ni Mwanachuo Mwita Nyarukururu na Mwenyekiti wa umoja huo, Mussa Omary
 Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Theodora Malata, akichangia jambo wakati wa kujibu maswali ya wanahabari.
 Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwanachuo Mussa Mashamba kutoka Chuo cha Ustawi wa Jamii, akisisitiza jambo wakati akijibu maswali ya wanahabari. Kulia Massoro Kivuga na William Haule. Dotto Mwaibale
 
”Sisi umoja wa vijana wa vyuo vikuu tunapinga vikali kauli hiyo na kulaani vikali ya kuhamasisha uasi kwa njia ya maandamano,”alisema.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa vijana hao Mussa Omary alisema kauli aliyotoa mwenyekiti huyo inahamasisha kuleta mgogoro nchini.
”Tumesononeshwa na kauli hiyo ya kibabe ya kiongozi huyu ya kuhamasisha vurugu ambazo tumezishuhudia zikisambaratisha umoja wa nchi nyingi na kuwa chanzo cha vita,”alisema.

”Tulimsikia akiahidi maandamano bila kikomo kwa kibali cha polisi au hata bila kibali cha polisi mbele ya wajumbe ambao wengine sio watanzania,”
Omari alisema uzito wa jambo hilo unaonesha wazi kuwa Mwenyekiti huyo hasatahili hata kidogo kuweza kupewa uongozi wa nchi hii.

”Wakiandaa maandamano haya huwa wanapiga picha na kuwatumia wafadhili wao na kupata fedha na kujenga majumba na kununua magari makubwa na huku watanzania wakiendela kuathirika,”alisema.
Alisema thamani ya mtanzania mmoja ni kubwa kuliko hiyo katiba mpya wanayodai ni vizuri watanzania kuacha kuwaunga mkono na kufanywa kama mbuzi wa kafara.
Aliongeza kuwa ni vyema vyombo vya dola visiweze kuvumilia kauli hiyo iliyotolewa hivyo kuendelea,kulinda kutunza na kuweza kuiendeleza amani ya nchi.

”Ni vizuri watanzania wakakaa na kufikiria kauli hii ya mwenykiti huyu na kujiuliza kuwa je ni kweli anaweza kuwa kiongozi wa nchi hii,”alisema.
”Sisi kama vijana wa vyuo vikuu msimamo wetu ni kuwa tuliachie bunge la katiba likafanya kazi yake na muda ukifika wa kutoa maoni yetu ukifika tutatoa maoni yetu na si kuvamia,”alisema

No comments: