Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba,Mhe. Hamad Rashid amewaomba viongozi kuheshimu na kutii sheria.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Mhe. Rashid wakati kikao cha Arobaini cha Bunge
hilo, kinachoendelea mjini Dodoma cha kujadili sura zote 15
zilizobakia za Rasimu ya Katiba Mpya, ikiwa ni mjadala wa mwisho.
“Hakuna
dhambi mbaya ya kuamrisha mtu kuvunja sheria. Ninaomba sana ndugu zangu
na viongozi wenzangu tutii sheria. Ndugu zangu tutulie tuendeshe nchi .
Hii nchi ina bahati ya ajabu,” alisema Rashid huku akisisitiza kuwa ina
Rais wa ajabu ambaye anaweza kumsikiliza mtu hata ambaye anampa amri.
Mhe.
Hamad aliwataka watu wasicheze na dola, huku akitolea mfano yeye na
wenzake 18 waliwahi kuwekwa ndani. Hivyo aliwaasa viongozi wenzake
wasicheze na Serikali, bali waitii.
Bunge
hilo, ambalo linaendelea kwa mujibu wa sheria, ambapo baadhi ya wajumbe
waliwataka wabunge wenzao kuendelea na kazi waliyotumwa na wananchi ya
kuhakikisha Katiba inayopendekezwa inapatikana Oktoba 4,mwaka huu.
No comments:
Post a Comment