Mhandisi
Hanifa Chingembe akielezea na kuonyesha kwa waandishi wa habari jinsi
mkongo wa Mawasiliano wa Taifa ulivysambaa nchi nzima.
……………………………………………….
(Picha na Hassan Silayo)
Frank Mvungi
Serikali imesema Mkongo wa Taifa umesaidia kushuka kwa gharama za mawasiliano kwa watumiaji wa mwisho nchini kutoka sh.147 kwa dakika mwaka 2009 hadi shilingi 62 kwa dakika mwaka 2013.
Hayo
yamesemwa na Msemaji wa Wizara ya Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya
Mawsiliano Sayansi na Teknolojia Bi Prisca Ulomi wakati wa mkutano na
waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Akifafanua
Bi Prisca amesema kuwa mkongo wa taifa umesaidia pia kushuka kwa
gharama za intaneti kutoka shilingi 36,000 hadi shilingi 9000/Gb kufikia
mwaka 2013.
“Mkongo
wa Taifa umesesaidia kuharakisha usambazaji wa huduma za mawasiliano
katika maeneo yasiyokuwa na mvuto wa kibiashara”alisisitiza bi Ulomi.
Katika
hatua nyingine, Bi Ulomi alisema faida nyingine ya Mkongo ni kuongezeka
kwa upatikanaji wa huduma za mawasiliano na uwezo wa kusafirisha
masafa.
Akieleza kuhusu gharama Bi Prisca amesema gharama za maunganisho ya mawasiliano ya simu za mkononi kutoka kampuni moja kwenda nyingine (interconnection fees) ambapo sasa gharama imepungua kutoka sh. 115 hadi shilingi 34.92 kwa dakika.
Mkongo wa Taifa umesaidia kuongeza ushirikiano wa kikanda kati
ya nchi za Afrika Mashariki na kati ambapo nchi za Rwanda, Burundi,
Zambia, Malawi, Uganda, na Kenya ambapo hali hiyo imeongeza fursa za
kibiashara na kukuza uchumi wa nchi.
Kufikia mwaka 2013 makampuni yafuatayo yalikuwa yameunganishwa na mkongo wa Taifa ni TTCL, TIGO, Zantel, Airtel, Vodacom, Simbanet na infinity.
No comments:
Post a Comment