Wednesday, September 3, 2014

SHIRIKA LA HUC LATANGAZA UFADHILI WA MASOMO YA UFUNDI VETA, VIJANA CHANGAMKIENI

Na Nathan Mpangala wa HUC
Shirika lisilo la kiserikali la Help for Underserved Communities Inc. (HUC), linatangaza nafasi za ufadhili wa masomo ya ufundi VETA kwa vijana wa Kitanzania. Kozi hizo ni ufundi wa magari, umeme wa magari, udereva magari/pikipiki, ufundi cherehani, hair dressing (urembo), mapambo ya ukumbi na nyinginezo  

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika hilo, inasema, HUC, itafadhili wanafunzi 15 wa kozi mbalimbali za awali VETA kwa mwaka 2014-2015.
Walengwa ni vijana wa kike na kiume waliomaliza shule za msingi ambao wamethibitika kuwa wazazi/walezi wao wameshindwa kuwalipia ada. Imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa, mwanafunzi atatakiwa kujaza kwa usahihi fomu ya maombi (imeambatanishwa hapa), akiambatanisha na barua akieleza sababu za kuomba ufadhili huu na barua ya utambulisho toka ofisi ya serikali za mitaa na mwisho wa kupokea barua za maombi ni Jumatano, Oktoba 01, 2014, saa 11 jioni. 

Barua za maombi zitumwe kupitia:
Maombi ya ufadhili wa masomo,
Help for Underserved Communities Inc.
P. O. Box 7022,
Dar es Salaam,
Tanzania.
Au
Help for Underserved Communities Inc.
P.O.Box 6822,
Ellicott City, MD 21042 
Au
Kupitia baruapepe:

No comments: