Thursday, September 11, 2014

OSCAR PISTORIUS HAJAKUTWA NA HATIA YA KUUA KWA KUKUSUDIA..LAKINI BADO ANAWEZA KWENDA JELA

Oscar Pistorius arrives at Pretoria Court on Thursday morning as he awaits verdict for murder trial
Oscar Pistorius akiwasili katika mahakama ya Pretoria leo mchana kusikiliza keshi inayomkalibi

JAJI anayeendesha kesi ya mauaji inayomhusu mwanariadha wa Afrika kusini, Oscar Pistorius, hajamkuta na hatia ya kumuua kwa kukusudia mpenzi wake, mwanariadha wa Olympic, Reeva Steenkamp
Katika kesi hiyo iliyosikilizwa leo, Jaji Thokozile Masipa alisema ushahidi wa kuthibitisha kuwa Pistorius, 27 aliua kwa makusudi haujajitosheleza kutoka kwa mwendesha mashitaka.
"Ushahidi wa kuhusika na mauaji, huo umejitosheleza" alisema Jaji, lakini hakutoa hukumu juu ya kesi hiyo ya Pistorius na kutoa wito kwa ajili ya chakula cha mchana mahakamani hapo.
Mbivu na mbichi zitajulikana leo hii.
Oscar Pistorius said he mistakenly shot Reeva Steenkamp on Valentine's Day in 2013
Oscar Pistorius alisema alimuua Reeva Steenkamp bila kukusudia katika siku ya wapendanao 'Valentine  Day' mwaka 2013.

Hata kama Pistorius hatakutwa na hatia ya kuua kwa kukusudia, bado anaweza kwenda jela kwa kosa la kumuua Steenkamp.
Mwanaridha huyo alikiri kutenda kosa hilo, lakini alisema hakukusudia.
Mashahidi wa utetezi walidai kuwa Pistorius alimuua kwa makusudi mpenzi wake kutokana na ugomvi uliotokea baina yao na majirani walisikia.
Reeva Steenkamp's mother, June (right), sits in the public gallery ahead of the verdict on Thursday
Mama yake Reeva Steenkamp, June (kulia), akiwa mahakamani hapo leo alhamisi
Post a Comment