Leo
September 11, 2011: Dunia inakumbuka tukio kubwa na baya la kigaidi
lilolofanywa na kundi la Al Qaeda chini ya uongozi wa Osama Bin Laden
mwaka 2001 baada ya kushambulia majengo ya kitengo cha ulinzi cha
Marekani jijini Washington na jengo la biashara huko New York na kuuawa
takribani watu 3,000.
Ilikuwa
siku ya Jumanne, September 11 mwaka 2001 ambapo kundi la kigaidi la Al
Qaeda chini ya uongozi wa Osama bin Laden liliteka ndege za Marekani,
American Airlines Flight 11 na United Airlines Flight 175 na
kuzigongesha kwenye matawi ya Kusini na Kaskazini ya jengo la ulinzi la
Pentagon, Washington na Jengo la Biashra 'World Trade Center Complex'
huko New York.
Ndege
nyingine zilizotekwa haziweza kutekeleza shambulizi na kulipuka wakati
abiria walipokuwa wanafanya jitihada za kujiokoa mikononi mwa watekaji.
Watu takribani 3,000 walipoteza maisha na kusababisha hasara ya zaidi ya takribani $ billion 10.
Osama Bin
Laden alithibisha kuwa kundi hilo ndilo lililotekeleza tukio hilo japo
alikanusha kuhusika na tukio la shambulizi la balozi za Marekani nchini
Tanzania na Kenya mwaka 2004.
Osama
alitaja sababu za kutekeleza tukio hilo kuwa ni uwepo wa vikosi vya
Marekani nchini Saudi Arabia na vikwazo ilivyowekewa nchi ya Iraq na
sapoti ya Marekani kwa Israel katika vita ya ukanda wa Gaza.
Shambulio
la September 11 lilikuwa shambulio baya la kigaidi katika historia ya
Marekani ambapo maafisa wengi zaidi na raia walipoteza maisha.
Marekani
ilianzisha mashambulizi makali nchini Afghanistan wakimsaka Osama Bin
Laden na vikundi vya Taliban vilivyokuwa vimemficha.
Vikosi vya Marekani vilimuua Osama bin Laden mwaka 2011 nchini Pakstani baada ya msako wa miaka 10.
No comments:
Post a Comment