Abiria hawa bila Kujali hatari wakiwa wanajipanga
kupanda katika Gari la Mizigo huku kukiwa na usafiri wa usalama na
wakutosha kabisa. Wakina mama wengine walikuwa na Watoto wao bila kujali
afya zao kwa kuwa barabara hiyo ilikuwa na vumbi la kutosha.
Askari wa usalama barabarani akiwa kazini
Askari wa usalama barabarani akitumia mamlaka yake kulisimamisha Gari lililoshehena Mizigo na Abiria Juu
Hata hivyo uchunguzi umebaini Bajaji kubeba abiria ili kulisubiria Lori mbele kama inavyo onekana Pichani.
Cha
Kushangaza zaidi hakuna abiria aliyeshushwa wala mizigo na kuamriwa
kuendelea na Safari , Je hapa tuseme ni usalama wa barabarani au ni
Hatari barabarani
Kwa Furaha Abiria walioshushwa na Bajaji wakisubiri Lori kwa matumaini ili kuendelea na Safari yao.
Safari inaendelea bila wasi wasi kila Lori na Safari yake na kwa nafasi
Mizigo Imesheena na abiria wamesheena
Safari
inaendelea bila wasi wasi ambapo Tulibaini kwa ukaribu kabisa Gari la
kwanza la Mizigo likipita Ishara kuonesha kuwa liliruhusiwa pasipo na
Pingamizi
Lori
la pili nalo linapita nalo bila wasiwasi , Tazama hapo juu huyo abiria
wa mbele alivyo jiegesha je Kuna tahadhari yotote hapa? Hapa pia
tulibaini Askari wa usalama wa barabarani aliliruhusu bila kipingamizi
Mistubishi ambayo tuliiona ikiwa
imesimamishwa na Askari wa usalama wa Barabarani nayo ikipita tena ikiwa
na watu wengi ndani yake mpaka wengine hawajakaa vizuri kama wanavyo
onekana
WAKATI
Serikali na wadau mbali mbali nchini wakihaha kuepusha ajali
zinazoendelea kuangamiza roho za watu, hali imekuwa tofauti kwa baadhi
ya madereva na wamiliki wa vyombo vya usafiri.
Ukiukwaji
wa sheria za usalama barabarani umejitokeza mara nyingi Barabara za
Mbeya-Chunya kupitia Kawetele na Mbeya-Mkwajuni Kupitia Mbalizi ambapo
yamekuwa yakibeba abiria na mizigo licha ya kuwepo mabasi yaliyoruhusiwa
Kisheria.
Mbeya
yetu imeshuhudia magari matatu aina ya Fuso na Scania kubeba mizigo na
kuning’iniza abiria juu jambo linalohatarisha usalama wa abiria na mali
zao.
Magari
hayo yalikutwa hivi karibuni yakitokea jijini Mbeya na kuelekea
Wilayani Chunya majira ya saa Tisa alasiri huku wasimamizi wa sheria za
usalama barabarani na Sumatra wakiyaruhusu kuendelea na safari licha ya
kuyaona yakifanya safari zake kila siku.
Mbeya
yetu ilishuhudia magari hayo yenye namba za usajili T 168AZG aina ya
Fuso, T 432 AAK aina ya Scania na T 646 BRQ aina ya Mitsubishi Fuso
yakiwa yanapita barabarani eneo la Mwansekwa na kuyashuhudia yakipita
Lwanjiro kwa ishara kuwa yaliruhusiwa kuendelea na safari.
Hata
hivyo usalama wa abiria hao umekuwa mashakani licha ya Serikali
kuimarisha barabara ya Mbeya-Chunya na kuwepo kwa magari ya abiria
Lukuki yanayofanya safari zake kila siku na Sumatra kuamua kupunguza
Gharama za usafiri. Ambapo awali walikuwa wakitozwa Tsh 10,000 kati ya
Mbeya na Chunya na sasa nauli imefikia hadi Tsh 5,000.
Hali
hii Hatari huwa mbaya zaidi wakati wa minada inayofanyika maeneo
mbalimbali katika Wilaya ya Chunya na Magari hiyo yamekuwa yakipita
pembezoni mwa kituo cha Polisi cha Wilaya hiyo.
JE WAHUSIKA MNALIONA HILI? NA TAMKO TUNANGOJA LITOLEWE HADI WAKATI WA MAAFA?
NDUGU MDAU KARIBU KUCHANGIA MAONI.
NA MBEYA YETU BLOG.
No comments:
Post a Comment