Mji wa Lusail uliopo umbali wa maili 9 kutoka mji
mkuu wa Doha huko Qatar ndio umepangwa kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la
Dunia mwaka 2022.
Sherehe za ufunguzi wa mashindano hayo makubwa
duniani ya mpira wa miguu na fainali zake zimepangwa kufanyika katika mji huo
tarajiwa utakao jengwa katika pwani ya Jangwa.
Qatar wapo wamesha toa michoro mbalimbali ya
majengo ya Hoteli, viwanja na maeneo mengine mbalimbali ya namna mji huo mpya
utakavyojengwa ili kukidhi mahitaji ya wageni katika fainali hizo.
Zaidi ya pauni bilioni 25 zinataraji kutumika
kujenga uwanja wa kisasa na waaina yake wa soka hapa duniani ambao utakuwa na
ukubwa wa takribani maili 28 za mraba na kuweza kumeza watu 86,000 watakao keti
vitini, huu si mwingine bali ni uwanja wa ‘Lusail Iconic Stadium’.
Endapo wahandisi watakamilisha kazi hiyo kwa
kiwango na ubora wa michoro kama inavyo onekana iliyotolewa mji huo utakuwa wa
kipekee na kivutio kikubwa cha utalii kwa Qatar.
Sehemu ya michoro hiyo upande gati za boti.
Uwanja wa soka wa ‘Lusail Iconic Stadium’. utakavyo kuwa.
Mandhari ya mji huo
No comments:
Post a Comment