Wednesday, September 10, 2014

PUMZIKA KWA AMANI UKO ULIKO RAFIKI YANGU GABRIEL MWASYEBULE NITAKUKUMBUKA DAIMA

MWEZI WA TATU MWAKA HUU NIKIWA NA RAFIKI YANGU GABRIEL MWASYEBULE WAKATI WA MAZIKO YA BABA YAKE MZAZI LAKINI LEO NI MWEZI WA TISA HAUPO NASI DUNIANI KWA KUPATWA NA KIFO KISICHOFIKIRIKA KABISA ULIPOUWAWA NA WATU UNAOKULA NAO,UNAOCHEKA NAO, UNAOISHI NAO, UNAO SALI NAO, HATA WANAKWAYA WAKO WALIKUKIMBIA AMBAPO ULIKUWA KATIBU WA VIJANA WA USHARIKA WA KKKT LWANGWA, HATA MCHUNGAJI WAKO NAYE? INAUMA SANA KUONA JAMII YAKO YOTE IMEKUHUKUMU UKIWA HAI HADI KUPATWA NA KIFO CHA AIBU CHA KUUWAWA KWA KUPIGWA NA VITU VYENYE NCHA KALI , MAWE, FIMBO,  NAJUA ULIPOKUWA KATIKA HARI MBAYA YA KUFIKIA MAUTI LABDA ULIPATA NAFASI YA KUONGEA NA MUNGU WAKO MIMI SIJUI LAKINI NINAIMANI MUNGU NI WA WATU WAKOSAJI NA SI WATAKATIFU KAMA BINADAM WANAVYOTAKA. PUMZIKA KWA AMANI UKO ULIKO RAFIKI YANGU GABRIEL MWASYEBULE NITAKUKUMBUKA KWA MENGI SANA HASA UPOLE NA UKARIMU WAKO MKE WAKO ROSTA NA WATOTO WAKO WATATU NAJUA UMEWAACHA KATIKA WAKATI MGUMU SANA LAKINI MUNGU TU ANAJUA JINSI YA KUWATUNZA.

INANIUMA SANA JINSI KIFO CHAKO ULIVYO JISHUHUDIA HADI UMAUTI UKUPATE NAJIULIZA NAFSINI MWANGU HIVI HAKUKUWEPO NA ADHABU NYINGINE YA KUMPA GABRIEL MWASYEBULE? KAMA NI MCHAWI JE NANI ANASHUHUDIA HILO HADHARANI? JE JAMII YOTE YA WATU WA LWANGWA KILA MTU ANAWEZA JISHUHUDIA NAFSINI MWAKE KAMA NI WASAFI? JE HUYU GABRIEL NDIO MCHAWI PEKE YAKE KAMA MNAVYOSEMA?
INAUMA SANA MOYONI MWANGU NASIKIA WATU WANAJISIFU KWEUPE KUWA BADO WATU WATATU MNAWAUA TENA
Post a Comment