Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kulima na kupanda mahindi katika shamba
kijijini Kwemnyefu Kata ya Mpapayu wilayani Mheza mkoani Tanga pamoja
na wananchi wakati alipotembelea shamba hilo na kukagua shughuli za
kilimo cha mkono, Katika shughuli hiyo katibu mkuu huyo ameshirikiana na
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi wakiwa katika ziara
ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na
kuhimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo, Katibu Mkuu
huyo kesho anaelekea wilayani Pangani baada ya kumaliza ziara yake
wilayani Muheza leo.
Nape
Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi naye akishiriki pamoja na
vijana kulima shambani katika kijiji cha Kwemnyefu wilayani Muheza leo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiendelea na kazi shambani pamoja na vijana wa kijiji cha Kwemnyefu kata ya Mpapayu
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi pamoja na vijana
wakirejea huku majembe yao yakiwa begani baada ya kumaliza kazi ya
kupanda mahindi shambani
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi pamoja na vijana wakirejea wakirejea huku majembe yao yakiwa beganibaada ya kumaliza kazi ya kupanda mahindi shambani
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Kilulu wilayani Muheza.
Jengo la Kituo cha habari za kilimo lililojengwa na serikali katika kata ya Songa wilayani Muheza ,Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana amelitembelea na kukagua ujenzi wa jengo hili.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa I. M.
Matovu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza wakati
alipotembelea kituo cha Afya Muheza na kukagua ujenzi wa miundo mbinu
kadhaa kabla kituo hicho hakijapandishwa hadhi na kuwa Hospitali ya
Mbaramo Ubwari wilaya ya Muheza.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Jitegemee mjini Muheza.
No comments:
Post a Comment