Kura ya maoni ya Katiba Inayopendekezwa itafanyika Machi 30 mwakani, gazeti hili limethibitisha.
Hayo
yalisemwa jana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick
Werema ambaye hata hivyo, alimwambia mwandishi wetu kwamba kabla ya kura
hiyo, "lazima daftari la kudumu la wapigakura liboreshwe kwanza" ili
kuwapa fursa wapigakura wapya ambao hawamo kwenye daftari hilo.
"Kuboreshwa
kwa daftari la wapigakura ni lazima kwa sababu kuna watu wengi
wamefikisha umri wa kupiga kura tangu tulipofanya uchaguzi mkuu na
hawamo kwenye daftari hilo, kwa hiyo hatuwezi kuwanyima fursa ya kupiga
kura kwa sababu ni haki yao kikatiba," alisema Jaji Werema na kuongeza:
"Lakini
lazima tujue pia kwamba kuboreshwa kwa daftari hilo kunahitaji fedha,
kwa hiyo kuboreshwa kwake kutategemea kama Serikali itatoa fedha kwa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ili kazi hiyo iweze kufanyika,
tusipoboresha daftari tutasababisha kelele na malalamiko mengi".
Msimamo
wa Jaji Werema ni sawa na ule wa Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva
ambaye amesisitiza mara kadhaa kwamba tume yake haitoandaa uchaguzi
wowote pasipo daftari la kudumu la wapigakura kuandikwa upya.
Jaji
Werema alisema ikiwa Serikali itatoa fedha, uboreshaji wa daftari
unaweza kukamilika ifikapo Februari 2015 na kwamba inatarajiwa kwamba
Machi 30, mwakani kura ya maoni itapigwa kama kila kitu kitakwenda kama
kilivyopangwa.
Alisema
upigaji kura utatanguliwa na kampeni ambazo zitafanyika kwa siku 30
kuanzia mwanzoni mwa Machi ili kushawishi Katiba inayopendekezwa iungwe
mkono au kinyume chake kwa makundi yanayoipinga.
Hadi sasa gharama za kusimamia kura ya maoni kwa ajili ya kupitisha Katiba Inayopendekezwa zimeendelea kuwa kitendawili.
Jana,
Jaji Lubuva alisema asingeweza kuzizungumzia kwa kuwa yuko Dodoma kikazi
na kuelekeza taarifa hizo zinaweza kupatikana kwa Mkurugenzi wa
Uchaguzi, Julius Malaba.
Hata
hivyo, alipotafutwa Malaba alisema anaweza kuzungumzia suala hilo katika
mkutano na waandishi wa habari anaotarajia kuuitisha wiki hii.
"Wiki hii
nitaitisha mkutano na waandishi wa habari kuhusu daftari la wapigakura.
Nadhani itakuwa vyema suala hilo likiibuliwa kupitia mkutano huo ndipo
majibu yanapoweza kupatikana," alisema.
Marekebisho ya sheria
CHanzo:Mwananchi
No comments:
Post a Comment