Sunday, October 12, 2014

TAIFA STARS YAILAZA NJAA BENIN, YAITANDIKA 4-1

Watu wengi walikuwa wakiibeza sana Stars kuelekea katika mchezo wa leo dhidi ya Benin, lakini ndiyo hivyo Wahenga walisema, “mdharau mwiba, mguu huota tende” na ndicho kilichowakuta Wa Benin leo katika dimba la taifa licha ya kusheheni nyota wengi wanaocheza soka la kulipwa barani Ulaya kama vile, Stephane Sesegnon anayekipa kunako West Bromwich Albion. 
Magoli ya Stars yalifungwa na beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Amri Kiemba, Thomas Ulimwengu, pamoja naye Juma Luizio. Goli la kufutia kijasho la Benin Lilifungwa na mshambuliaji Sadel akipokea pasi maridadi kutoka kwake kiungo mshambuliaji, Stephane Sesegnon dakika ya 90 ya mchezo huo.
Ushindi huo ni furaha kubwa kwa watanzania ambao walikuwa wamekata tamaa na timu yao ya taifa iliyopo chini ya kocho Mholanzi Mart Nooij kufuatia matokeo mabovu ya hivi karibuni katika michuano ya kuwania tiketi za kupangwa katika makundi ya michuano ya AFCON yatakayo fanyika mwakani nchini Moroco..
Post a Comment