Sunday, October 12, 2014

VIJANA WATATU WA TUKUYU WILAYANI RUNGWE WAFA MAJI KATIKA ZIWA NYASA

MAREHEMU NOAH SANGA ENZI ZA UHAI WAKE ALIKUWA NI DEREVA WA PIKIPIKI KIJIWE CHA BAGAMOYO SOKO LA BUJINGA

MAREHEMU MARCK EMMANUEL ENZI ZA UHAI WAKE AMBAYE ALIKUWA ANAISHI NA WAZAZI WAKE MTAA WA KIWIRARODI TUKUYU MJINI MAZIKO YANAMSUBIRI BABA YAKE MZAZI AMBAYE YUPO SAFARINI AFRIKA YA KUSINI

MAMA MZAZI WA NOAH SANGA AKILIA KWA UCHUNGU BAADA YA KUFIWA NA MWANAE WA KWANZA KATIKA ZIWA NYASA

AKIWA NA MAJONZI BABA MZAZI WA NOAH SANGA

SHUHUDA WA KIFO KILIVYO TOKEA RAUBEN KYANDO AMESEMA KUWA MNAMO TAREHE 09.10.2014 MUDA WA ASUBUHI AKIWA NA WENZAKE WAENDESHA PIKIPIKI NANE WAKIWA NA ABILIA WAO AMBAO WALIKODISHA PIKIPIKI NA KUWAPELEKA MATEMA KWA AJILI YA MAPUMZIKO YA SIKU. WAKIWA KATIKA MAPUMZIKO WAKIWA UFUKWENI WALIPEWA TAARIFA YA KUWA ZIWA NYASA LIMECHAFUKA HIVYO WASIINGIE KUOGELEA LAKIN BAADA YA MUDA WALIPATA NAFASI YA KUOGA KWA UANGALIFU PEMBEZONI LAKINI BAADA YA MASAA MATATU KUPITA WAKARUDI TENA MAJINI KUOGELEA  NDIPO WAKIWA KATIKA HARI YA KUOGELEA WENZAKE WANNE WAKAZIDIWA NA MAJI NA YEYE RAUBEN AKIWA NDIYE MTU PEKEE ANAYEWEZA KUOGELEA AKAFANIKIWA KUMUOKOA BINTI MMOJA AITWAYE SEKELA MKAZI WA TUKUYU NA HUKU MAJINI WAKIBAKI WATU WATATU AMBAPO ALIPORUDI TENA HAKUFANIKIWA KUWAOKOA KWAKUWA WALIZIDIWA NA MAJI AMBAPO ZIWA LILIKUWA LIMECHAFUKA ZAIDI. BAADA YA MASAA MATATU KUPITA WATU WATATU WALIKUFA MAJI KATIKA ZIWA NYASA NA MAITI ZAO KUSAFIRISHWA HADI CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI TUKUYU. MAREHEMU WAWILI WAMEZIKWA TAYARI ILA MMOJA MACK EMMANUEL MAZIKO YANASUBIRI KUWASILI KWA BABA MZAZI ALIYEYO SAFARI AFRIKA YA KUSINI

KULIA MHE, HILDA NGOYE MBUNGE ALIKUWEPO MSIBANI KUSHIRIKI KUOMBOLEZA MSIBA WA NOAH SANGA AMBAPO MAMA MZAZI WA NOAH NI MFANYAKAZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM WILAYA YA RUNGWE

KUSHOTO ALLY MWAKALINDILE MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA RUNGWE AKIWA NA KATIBU MWENEZI WA CCM WILAYA YA RUNGWE WAKITETA JAMBO KATIKA MSIBA WA NOAH SANGA

WAOMBOLEZAJI WAKIWA MSIBANI BAGAMOYO  TUKUYU

BAADHI YA WAOMBOLEZAJI

BAADHI YA WARATIBU WA MAZIKO AMBAPO MAZIKO YANAFANYIKA WILAYA YA MAKETE

NDUGU NA JAMAA WAKIJADIRI JINSI YA KUSAFIRISHA MAITI KWENDA MAKETE IRINGA KWA AJILI YA MAZIKO

MAITI YA NOAH IKITOLEWA NDANI NA KUELEKEA KWENYE GALI NA KUANZA SAFARI YA KWENDA MAKETE KWA MAZIKO

BAADHI YA WENZAKE NA MAREHEMU WAKIJIANDAA KWA AJILI YA MAANDAMANO YA KUSINDIKIZA MWILI WA MAREHEMU NOAH KWENDA WILAYANI MAKETE

MAMA MZAZI WA NOAH SANGA AKILIA KWA UCHUNGU


GALI YA CCM WILAYA YA RUNGWE IKIWA IMEBEBA JENEZA LA MAREHEMU KUELEKEA WILAYANI MAKETE HUKU UONGOZI WA CCM WILAYA YA RUNGWE WAKIONGOZA MSAFARA HUO WA MSIBA

Post a Comment