Thursday, October 9, 2014

OFISI YA BONDE LA MAJI ZIWA NYASA LA DHAMINI MCHEZO WA MIGUU WILAYANI RUNGWE KWA TIMU 16 AMBAPO SASA MTANANGE UKO HATUA YA NUSU FAINALI MCHEZO KATI YA KATUMBA & LUTENGANO NA NUSU FAINALI YA PILI NI TUKUYU STARS & JUHUDI HUKU FAINALI IKITARAJIWA KUSHUHUDIWA NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DR JAKAYA KIKWETE LENGO LIKIWA NI JUHUDI ZA KUTUNZA NA KUHIFADHI MAZINGIRA NA VYANZO VYA MAJI

MAKAO MAKUU YA OFISI YA BONDE LA MAJI KWA MIKOA MITATU MKOA WA MBEYA , MKOA WA NJOMBE NA MKOA WA RUVUMA PAMOJA NA WILAYA KUMI NA TATU AMBAZO NI RUNGWE MAKAO MAKUU YA OFISI NA IKIWA NDIO SEHEMU PEKEE YENYE VYANZO VYA MAJI VINGI NA UHAKIKA. MBEYA VIJIJINI, ILEJE, MOMBA, KYELA, MAKETE, NJOMBE NA LUDEWA, SONGEA, NANTUMBO, MBINGA NA NYASA

KUSHOTO NI AFISA MAJI WA BONDE LA ZIWA NYASA AKIWA NA ENG INNOCENT LYAMUYA WAKIWA  OFISIN  WAKIENDELEA NA MAJUKUMU YAO YA KAZI AMBAPO MAKAO MAKUU YA OFISI YA BONDE LA ZIWA NYASA LINATARAJIWA KUZINDULIWA NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DR  JAKAYA KIKWETE ATAKAPO FANYA ZIARA WILAYANI RUNGWE HIVI KARIBUNI

MUONEKANO WA JENGO LA OFISI YA MAKAO MAKUU YA BONDE LA ZIWA NYASA OFISI ILIYOPO KATIKA WILAYANI RUNGWE MKOA WA MBEYA

MAKAO MAKUU YA BONDE LA ZIWA NYASA

AFISA MAJI BONDE LA ZIWA NYASA WITGAL NKONDOLA AMESEMA KUA MBINU MBALIMBALI ZA KUFIKISHA UJUMBE KWA WANANCHI WA RUNGWE NA SEHEMU ZINGINE ILI KUJUA UMUHIMU WA UTUNZAJI WA MAZINGIRA NA VYANZO VYA MAJI KWA MANUFAA YA KIZAZI CHA SASA NA KIJACHO, HIVYO KWA SASA WANATUMIA MICHEZO HASA MCHE ZO WA MPIRA WA MIGUUA MBAPO TIMU KUMI NA SITA ZILIANZA MASHINDANO AMBAPO HADI SASA MASHINDANO YAPO KATIKA NGAZI YA NUSU FAINALI AMBAZO LEO TIMU YA LUTENGANO STARS IMEICHABANGA KATUMBA STARS MAGOLI MAWILI KWA NUNGE AMBAPO FAINALI ITACHEZWA MWEZI UJAO AMBAPO ENG NKONDOLA ANASEMA FAINALI ITACHEZWA KATIKA SIKU YA KILELE CHA UZINDUZI WA JENGO LA KISASA LA OFISI YA BONDE LA MAJI LILILOJENGWA NA SERIKALI  AMBAPO MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DR JAKAYA KIKWETE AKIWA ZIARANI MBEYA ATAZINDUA JENGO LA MAKAO MAKUU YA BONDE LA MAJI LILILOPO WILAYANI RUNGWE MKOA WA MBEYA

MCHEZO UKIENDELEA

KUANZIA KULIA NI AFISA WA MAJI WA BONDE LA ZIWA NYASA ENG WITGAL DANIEL NKONDOLA, INNOCENT LYAMUYA, AYOUB CHANGALIMA (MHASIBU) NA HUSEIN MAHABA MHASIBU WA BONDE LA MAJI WAKIFUATILIA KWA MAKINI MTANANGE WA NUSU FAINALI KATI YA TIMU YA KATUMBA STAR NA LUTENGANO FC AMBAPO HADI FILIMBI YA MWISHO LUTENGANO STAR WAMEIBUKA WASHINDI KWA MAGOLI MAWILI KWA NUNGE

TIMU YA LUTENGANO WAKIWA MAPUMZIKO KATIKA SEHEMU YAO YA KUPUMZIKIA WAKIPEANA MAWAIDHA BAADA YA KUFUNGWA GOLI MOJA KWA BILA HADI MAPUMZIKO


BAADHI YA WAZEE MAARUFU WA TUKUYU WAKIFUATILIA KWA UMAKIN MCHEZO WA NUSU FAINALI KATI YA LUTENGANO STARS NA KATUMBA STARS

BAADHI YA MASHABIKI WALIOJITOKEZA KUJIONEA MTANAGE WA NUSU FAINALI IKIWA NI SEHEMU PIA YA KUPATA ELIMU YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA HASA KATIKA VYANZO VYA MAJI ELIMU INAYOTOLEWA NA OFISI YA BONDE LA MAJI AMBAYO INA MAKAO MAKUU MJINI TUKUYU WILAYANI RUNGWE

BAADHI YA MASHABIKI WALIOJITOKEZA KUJIONEA MTANAGE WA NUSU FAINALI IKIWA NI SEHEMU PIA YA KUPATA ELIMU YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA HASA KATIKA VYANZO VYA MAJI ELIMU INAYOTOLEWA NA OFISI YA BONDE LA MAJI AMBAYO INA MAKAO MAKUU MJINI TUKUYU WILAYANI RUNGWE

WADAU WA MICHEZO WAKIPATA POZI LA PICHA HUKU WAKIENDELEA KUANGALIA MCHEZO WA NUSU FAINALI

WADAU WA MICHEZO WAKIJADIRI MAMBO HUKU WAKIENDELEA KUANGALIA MPIRA

MOJA YA MBINU ZA KUENEZA UJUMBE WA UTUNZAJI WA MAZINGIRA NA KUHIFADI VYANZO VYA MAJI NI KUWEKA MABANGO KATIKA MITAA NA NJIA KUU ILI UJUMBE KUWAFIKIA WATU MBALIMBALI

ENG WITGAL NKONDOLA  AMESEMA KUWA MBINU MBALIMBALI ZA KUWAFIKIA WADAU WA MAJI NA WATU MBALIMBALI ZINAFANYIKA ILI ELIMU ITOLEWAYO YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA NA KUHIFADHI VYANZO VYA MAJI ZINATUMIKA NI PAMOJA NA  KUWEPO KWA MIKUTANO YA HADHARA KATIKA VIJIJI HUSIKA, MICHEZO NA NGOMA ZA KIENYEJI ILI KUFIKISHA UJUMBE KWA UMAKINI  PIA KUTOA ELIMU MASHULENI ILI WANAFUNZI KUPATA ELIMU YA KUTAMBUE UTUNZAJI WA VYANZO VYA MAJI KWA AJILI YA KIZAZI CHA SASA NA KIZAZI KIJACHO
KINGOTANZANIA
Post a Comment