Meneja wa Maabara kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) Mhandisi Mvunilwa Mwarabu akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) mashine ya kupimia kiwango cha madini inayoitwa Atomic Absorption Spectroscopy (AAS) walipotembelea Maabara ya Wakala huo jijini Dar es Salaam jana.
Mkemia Alfred Aloyce kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) sampuli ya jiwe la dhahabu iliyotayarishwa kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kimaabara ili kubaini kiasi cha madini ya dhahabu kwenye jiwe hilo.
Madini ya ujenzi aina ya kokoto zilizo tayari kwa matumizi ya ujenzi wa aina mbalimbali. Kupitia TMAA Madini hayo kwa sasa yanaipatia Serikali zaidi ya shilingi bilioni 5 kwa mwaka.(Martha Magessa)
Waandishi wa habari waliotembelea ofisi za Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) wakipata maelezo kuhusu mafanikio ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini katika ukusanyaji wa mirabaha ya madini kutoka kwa Mkurugenzi wa Fedha wa wakala huo Bw. Bruno Mteta.
Kaimu
Mkurugenzi Uzalishaji na Usafirishaji kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini
(TMAA) Bw. Conrad Mtui akiwaeleza waandishi wa habari mikakati ya
ukusanyaji wa mirabaha ya madini ya ujenzi wakati walipotembelea kituo
cha ukaguzi wa madini hayo kilichopo wilayani Bagamoyo.
Mashine
ya Kuyeyusha sampuli za Madini(Fusion and cuppelation Funances)
inayotumika kwenye Maabara ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA)Picha na Fatma Salum-MAELEZO
Georgina Misama-MAELEZO
Wakala wa
Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) imeiwezesha Serikali kukusanya
mrabaha wa jumla ya shilingi billioni 5.2 tangu kuanzishwa kwa wakala
huo.
Hayo
yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi uzalishaji na usafirishaji wa madini Bwn
Conrad Mtui wakati wa ziara ya waandishi wa habari walipotembelea migodi
ya Lugoba na Msolwa Chalinze, hivi karibuni
"Wakala
umefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi bilioni 5.2 kutokana na madini
hayo yaliyozalishwa na kuuzwa na wamiliki halali wa leseni katika mikoa
mbalimbali kwenye kanda za Kaskazini, kati, Kusini, Kusini Maghalibi,
Maghalibi, Mashariki na Ziwa Victoria" alisema Mtui
Aidha,Wakala
kwa kushirikiana na Ofisi za Madini ulibuni matumizi ya "Hati ya Mauzo"
kwa lengo la kudhibiti shughuli za uzalishaji na mauzo ya madini,
mkakati ambao ulianza kutumika mwezi Juni, 2011 utakaohusisha Mikoa ya
Dar es Salaam na Pwani
Pia,
Wakala ulifanya ukaguzi na uhakiki wa madini yaliyozalishwa na kuuzwa na
migodi mikubwa ya madini nchini, ikiwa na lengo la kupata mrabaha na
takwimu sahihi za madini yaliyozalishwa na migodi hiyo.
Akitaja
migodi iliyofanyiwa ukaguzi alisema ni Mgodi wa dhahabu wa Geita, Golden
Pride, Bulyanhulu, Tulawaka, North Mara, Buzwagi na New Luika
iliyowezesha kukusanywa kwa jumla ya Dola za Marekani milioni 427.98
Akizungumzia
kuhusu hatua wanazochukuliwa baadhi ya wamiliki wa migodi wanaokiuka
taratibu za "Hati ya Mauzo" Mkaguzi wa Madini ya Ujenzi na Viwandani
Abubakari Jihango alisema kuwa hadi sasa kuna kuna kesi 53 mahakamani,
na kama itadhihirika ukiukwaji wa sheria, taratibu za kisheria
zitafuatwa.
No comments:
Post a Comment