Bw.Hassan Mtenga
CHAMA cha mapinduzi (CCM) mkoa
wa Iringa chakishangaa chama cha demokrasia na maendeo (CHADEMA) kwa
kuwazuia wanachama wake mjini Iringa kunywa maziwa ya
Asas Dairies Ltd
Akizungumza na waandishi wa
habari ofisini kwake jana katibu wa CCM mkoa wa Iringa Hassan
Mtenga alisema kuwa hatua ya Chadema kuwazuia wanachama wake
mjini Iringa kunywa maziwa ni dalili mbaya kwa mbunge wa jimbo la
Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa mwaka 2015.
Kwani alisema kuwa kuwazuia
wanachama wao kunywa maziwa ni moja ya hatua ya kuwataka kufa kabla
ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 kwani maziwa ni tiba tosha kwa watu
wenye matatizo na wasio na matatizo.
Mtenga alisema kuwa maziwa
ya Asas Dairies Ltd hayana uhusiano wowote na chama chochote cha
siasa na kuwa hatua ya viongozi wa chadema kuacha kuzungumzia
kazi ambazo mbunge wao Msigwa amefanya na kuelekeza mapambano yake
katika maziwa si siasa bali ni kuishiwa hoja za kuwaeleza
wananchi.
“Tunashangazwa sana na uwezo
wa uelewa wa viongozi wa Chadema hivi kweli inaingia akilini kiongozi
ama chama kumzuia mwanachama wake kunywa maziwa ama kula ? kweli
ni kufirisika kisera maana bila mtu kula atakufa na nani atakupigia
kura ” alihoji Mtenga
Hata hivyo alisema kuwa
hakuna asiyetambua kuwa wapo wafanyabiashara ambao ni wanachama wa
Chadema kama hivyo ndivyo basi CCM kuwatangazia wanachama wake
kuwa wasinunue wala kuingia katika maduka ama kupenda bidhaa za
wafanyabiashara ambao ni wanachama wa Chadema nchini.
Alisema kuwa kuwa kawaida
chama kina mpaka yako katika kuwaongoza wananachi na wananachi ama
wanachama wana uhuru wa kupenda chochote bila kuvunga sheria .
Hivyo alisema kuwa chadema
wanapaswa kuwaomba radhi wananchi wa jimbo la Iringa kwa kauli hiyo
ambayo ni sawa na kumzuia mtu kula ama kuishi vinginevyo CCM
kinawataka wananchi kupuuza kauli hiyo ambayo imelenga kuwaondolea
haki ya kuishi .
Pia alisema iwapo wanachama
wana biashara zao si vema vyama kuhusisha biashara ya mtu na itikadi
za vyama na kudai kuwa viongozi wa chama wapo kwa ajili ya kuvuruga
biashara za watu .
CCM kimetoa kauli baada ya
viongozi wa chadema Iringa mjini na makamu mwenyekiti wa baraza la
vijana Taifa (BAVICHA ) Patrick Sosopi kutumia mkutano wake wa hadhara
kuwazuia wananchi kunywa maziwa hayo ya asas kwa kudai kuwa mmoja
kati ya wanafamilia wa mmiliki wa kampuni hiyo anasaidia CCM Iringa .
No comments:
Post a Comment