Ndoa ya mashoga
Makundi
ya kikatoliki yanayopigania haki za wapenzi wa jinsia moja yameelezea
ghadhabu yao kutokana na hatua ya maaskofu wa kanisa hilo ya kukataa
mapendekezo ya kutangaza msimamo kuhusu mashoga, wasagaji pamoja na watu
waliotalakiana na wanaoana.
Wakati wa
kumalizika kwa mkutano wa maaskofu wa kanisa katoliki, Vatican
ilishindwa kupata theluthi mbili ya kura za maskofu wa kuunga mkono
maoni yao kuhusu masuala hayo.
Kundi la
kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja nchini Marekani la New Ways
Ministry limesema kuwa hatua ya maskofu hao kuamua kujadili suala hilo
ni matumaini ya siku za usoni.
Masuala hayo yanatarajiwa kuzungumziwa tena baada ya mwaka mmoja. BBC
No comments:
Post a Comment