Rais Kikwete akutana na Rais Kabila Arusha
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikiwete akizungumza na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri
ya kidemorasia ya Kongo DRC muda mfupi kabla ya marais hao wawili
kuongoza sherehe za kutunuku kamisheni na kuhitimu mafunzo kwa maafisa
wapya wa jeshi kutoka katika nchi hizi mbili jirani.Sherehe hizo
zilifanyika katika chuo cha kijeshi Monduli mjini Arusha leo
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya
kidemokrasia ya Kongo DRC wakiwa katika sherehe ya kuhitimu mafunzo ya
maafisa wanafunzi kundi la 54/13 kutoka Tanzania na DRC. DRC katika chuo
cha Mafunzo ya kijeshi kilichopo Monduli Mkoani Arusha leo.
Amiri
Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Joseph Kabila wa DRC na
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wakijadili jambo wakati wa
hafla ya kuhitimu mafunzo na kutunuku kamisheni kwa maafisa wa kundi la
54/13 DRC yaliyofanyika chuo cha kijeshi Monduli Mkoani Arusha
jana.(picha na Freddy Maro)
Rais
Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) akimpa zawadi
ofisa kadeti Yusup kutoka DRC baada ya kuibuka mwanafunzi bora katika
kundi la 54/13 wakati wa hafla ya kumaliza mafunzo iliyofanyika huko
Monduli jana.
Rais
Joseph Kabila wa DRC akimpa zawadi Ofisa Kadeti Ibrahim Mwamtemi baada
ya kuibuka mwanafunzi bora katika mafunzo ya porini wakati wa hafla ya
kutunuku kmaisheni baada kumaliza mafunzo ya kundi la 54/13 DRC
yaliyofanyika Chuo cha kijeshi monduli jana.
Amiri
Jeshi Mkuu, Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitunuku kamisheni kwa
maofisa wa Jeshi wanafunzi kundi la 54/13 DRC katika chuo cha Mafunzo ya
kijeshi kilichopo Monduli Mkoani Arusha jana.
Maafisa
wapya wa jeshi la Wananchi wa Tanzania wakila kiapo cha utii kwa Amiri
Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa hafla ya kutunuku
kamisheni kwa maafisa wapya wa jeshi la wananchi wa Tanzania
iliyofanyika katika chuo cha mafunzo ya kijeshi kilichopo Monduli Mkoani
Arusha jana.
No comments:
Post a Comment