Thursday, December 11, 2014

Ebola bado tishio Sierra LeoneShughuli za mazishi hufanywa kwa makini kuepuka maambukizi ya Ebola
Maafisa wa Afya nchini Sierra Leone wamegundua miili kadhaa katika maeneo ya mgodi wa Almasi, na kusababisha hofu kuwa pengine ugonjwa wa Ebola haujaripotiwa ipasavyo.
Shirika la afya duniani,WHO limesema limebaini kisa hiki kipya mashariki mwa mji wa Kono, timu ya Wataalamu imepelekwa Kono kufanya uchunguzi kuhusu uwepo wa ugonjwa wa Ebola.
Watu 6,346 wamepoteza maish akutokana na ugonjwa huo na zaidi ya 17,800 wameathirika na Ebola.BBC
Post a Comment