Tuesday, December 2, 2014

KINANA AANDIKA HISTORIA MIKOA YA LINDI NA MTWARA

ZIARA YA KINANA MIKOA YA LINDI NA MTWARA YAINGIZA  WANACHAMA ZAIDI YA 40,000 CCM
Wakazi wa Mtwara mjini wakishangilia wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM ukiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Mtwara mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa kazi ya CCM ni kuisimamia Serikali kutimiza wajibu wake kwa wananchi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mtwara mjini na kuwaa
 Mbunge wa Mtwara Mjini Ndugu Hasnain Murji akieleza utekelezaji wa ilani ya CCM ulivyotekelezwa vizuri kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa ambapo pia alieleza changamoto zinazowakabili wananchi wa Mtwara mjini hivyo kumtaka Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kusaidia katika kufanikisha baadhi ya mambo ambayo yameonekana kukwamishwa na viongozi wa juu serikalini.
 Wananchi wakilizunguka gari alilopanda Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kumaliza kuhutubia kwenye viwanja vya Mashujaa Mtwara mjini.
MAPOKEZI YA KINANA MTWARA MJINI
  Vijana wa Bodaboda wakiongoza msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akiwasili Mtwara mjini ambapo alishiriki shughuli mbali mbali za kujenga na kuimarisha chama pamoja na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010.
     Msafara wa Katibu Mkuu ukielekea Mtwara mjini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mikindani mara baada ya kukabidhi leseni kwa madereva 70 wa boda boda waliohitimu mafunzo chini ya udhamini wa Mbunge wa Mtwara mjini Hasnain Murji.
                                                   MTWARA VIJIJINI
 Wananchi wa kijiji cha Kitaya mkoani Mtwara wakishangilia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye kijiji hicho kinachopakana na nchi ya Msumbiji.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Kitaya kilichopo mpakani na nchi ya Msumbiji ikiwa sehemu ya ziara yake mkoani Mtwara ambapo anakagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi pamoja na kujenga na kuimarisha chama.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa kata ya Nanguruwe ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa kuna sheria zinazomkandamiza mkulima inabidi zitazamwe upya kwani zisipobadilishwa mkulima atakuwa anakandamizwa kila siku na kutoona faida ya kuwa mkulima wa korosho.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa kata ya Nanguruwe wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM kwenye wilaya ya Mtwara Vijijini,tarehe 28 Novemba 2014.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye mnara wa shujaa Ahamad Mzee aliyepambana na Wareno waliokuwa wanataka kuivamia Tanzania mwaka 1972 mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.
                                                          TANDAHIMBA
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Tandahimba ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa zao la korosho lina hadithi nyingi sana na njia pekee ya kuleta ukombozi kwa mkulima ni kujenga kwa viwanda vya kutosha vya kubangulia Korosho nchini pia aliwataka wazazi wa Tandahimba kusisitiza elimu kwa watoto wao kwani ndio mkombozi pekee atakayekuja kuwakomboa kwenye maisha yao.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Tandahimba ambapo aliwaambia wasihadaike na wapinzani ambao muda wao wa ujana wameutumia wakiwa CCM na uzeeni kuingia upinzani na kuanza kuhadaa watu walioishi kwa amani kwa muda mrefu.
  Wananchi wa Tandahimba mkoani Mtwara wakifuatilia kwa makini hotuba za viongozi wa CCM wakiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye anazunguka nchi nzima kukagua na kuimarisha uhai wa Chama.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kata ya Mndimba wakati waujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Mdimba wilayani Tandahimba.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi zilizorudishwa na wapinzani kata ya Mdimba wilaya ya Tandahimba.
                                                   NEWALA
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwaonyesha wananchi wa Mkwedu kadi ya CUF iliyorejeshwa kwake na Hakika Ibrahim ambaye alirudisha kadi hiyo baada ya kuona na kuelewa utekelezaji wa ahadi za CCM unavyokwenda vizuri.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionnyesha kadi juu zilizorudi kutoka upinzani ambapo wanachama hao kutoka upinzani wameahidi kushirikiana na CCM kwa ajili ya kuleta maendeleo yaTengulengu wilayani Newala.
 Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Newala Ndugu  Adam Lawi Nangwanda Sijaona akivua nguo za Chadema mbele ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye.
 Wananchi wakishangilia kurejea kwa  Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Newala Ndugu  Adam Lawi Nangwanda Sijaona kwenye mkutano wa hadhara uuliofanyika kwenye viwanja vya Mahakama ya mwanzo Newala
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Newala kwenye viwanja vya Mahakama ya Mwanzo ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa Serikali lazima itafute namna ya kuhakikisha uzalishaji wa korosho wote unafanyika nchini kwa kujenga viwanda vya kutosha vya korosho.
Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Newala Ndugu  Adam Lawi Nangwanda Sijaona akiwa amekabidhi kadi yake na ya mkewe kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .
                                                       NANYUMBU
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mangaka  wilaya ya Nanyumbu ambapo aliwaambia CCM ya sasa itakuwa kali kuliko wakati wowote na itaisimamia serikali na kuipongeza inapofanya vizuri na itakapofanya vibaya itasemwa.

No comments: