Tuesday, December 2, 2014

ITV YAZINDULIWA DSTV

images
MultiChoice Africa, kampuni inayoongoza katika kutoa burudani ya kulipiwa ya dijitali pamoja na IPP Media wamesaini makubaliano yatakayoleta chaneli maarufu zaidi Tanzania, ITV, kuwa sehemu ya jukwaa la DStv.
Ushirikiano huu wa kusisimua utawapa watazamaji wa Tanzania kote nchini fursa ya kuangalia vipindi vilivyotengenezwa hapa hapa nchini vikiwa na ubora mkubwa kidijitali. Chaneli hii itapatikana kwenye vifurushi vyote vya DStv ikiwemo kifurushi kilichozinduliwa hivi karibuni cha Bomba, Family, Compact, Compact Plus na Premium.
Akizungumzia ushirikiano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa ITV Bi Joyce Mhaville alisema: “Tunajivunia sana ushirikiano huu ambao tumekuwa tukiufanyia kazi kwa muda mrefu. Fursa zinazojitokeza kutokana na makubaliano haya yatanufaisha kampuni zote mbili pamoja na kuwanufaisha watazamaji wetu, hasa kwa wakati huu ambao tumehama kutoka katika mfumo wa analojia kuingia dijitali. ITV ina vipindi vyenye ubora vilivyotengenezwa hapa hapa nchini na ambavyo vinawafaa watanzania wakati DStv itatuwezesha kupanua wigo wetu.”
Akizungumza juu ya hili, Mkurugenzi wa MultiChoice Africa kanda ya Afrika Mashariki Bwn Stephen Isaboke alisema: “MultiChoice imejizatiti kuwapa watazamaji wake chaneli nyingi mbalimbali zikiwepo zinazoonyesha vipindi vya hapa hapa na vile vya nje. Kwa kuwa ITV inakuwa kwa kasi na ina watazamaji wengi, ushirikiano huu utatufaa kwa vile unaongeza vipindi vilivyotengenezwa hapa nchini. Tutaendelea kuwekeza katika kuwaletea vipindi vyenye utofauti. Kwa kupitia vifurushi vyetu mbalimbali, tunawapa wateja wetu chaneli nyingi kwa bei tofauti ili wawe na uwanja mpana wa kuchagua.”
Bw Isaboke na Bi Mhavile walionyesha kufurahishwa sana na kujitoa kwao kwa ushirikiano huu. Waliwahamasisha watanzania kununua DStv ili waweze kufurahia ITV na chaneli zingine nzuri.
Post a Comment