Tuesday, December 30, 2014

KOCHA PATRICK PHIRI AFUKUZWA SIMBA


index
PATRICK PHIRI

Klabu ya simba imemfukuza kocha PATRICK PHIRI kutokana na kutoridhishwa na matokeo mabaya ya timu hiyo.
Kocha huyo Mzambia amekuwa hana matokeo mazuri tangu ajiunge na timu hiyo Agosti mwaka huu akirithi mikoba ya ZDARVKO LOGARUSIC kutoka Croatia.

PHIRI ameiongoza Simba kwa mara ya mwisho Dec 26 katika mchezo wa ligi kuu waliofungwa 1-0 na timu ya Kagera Sugar.

Hii ni mara ya tatu kwa Phiri kuifundisha Simba na tangu ajiunge na timu hiyo August mwaka huu ameiongoza katika michezo 22 na kushinda nane ,kati ya hizo ni moja tu ya ligi kuu na moja ya nani mtani jembe.
Aidha taarifa zinasema kuwa Mserbia GORAN KOPUNOVIC atawasili nchini kesho jumatano ili kuchukua mikoba ya PHIRI.

Hata hivyo KOPUNOVIC anatarajiwa kusaidiwa na mnyarwanda JEAN MARIE NTAGAWABILA kwa maana aliyekuwa msaidizi wa PHIRI,SULEIMAN MATOLA naye.
ataondolewa katika nafasi hiyo.

KOPUNOVIC alifanya kazi kwa mafanikio nchini Rwanda akiwa na klabu ya Polisi kwa miaka mitatu kabla ya kuhamia Vietnam ambako pia alifanya kazi kwa mafanikio.
Post a Comment