Thursday, December 25, 2014

MGENI RASMI WAZIRI MKUU MSTAAFU FREDRICK SUMAYE AWASILI JIJINI MBEYA, TAYARI KWA KUONGOZA TAMASHA LA KRISMAS

Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akiwasili  na ndege ya shirika la ndege la Fastjet kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe mjini Mbeya huku akiwa ameongozana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste nchini (CPCT), Askofu David Mwasota kushoto na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama Tayari kwa kuhudhuria Tamasha la Krismas ambalo linafanyika kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Mh, Sumaye atakuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo ambalo litashirikisha waimbaji wengi kutoka hapa nchini na nchi jirani. 2 
Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama  wakifurahia jambo kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste nchini (CPCT), Askofu David Mwasota na MC Mwakipesile. 5 
MC. Mwakipesile kulia na John Melele mmoja wa waratibu wa Tamasha hilo wakifurahia jambo kwenye uwanja wa Ndege wa Songwe mkoani Mbeya.
Post a Comment