TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 21.12.2014
MAJIRA YA SAA 14:10 MCHANA HUKO
KATIKA KIJIJI CHA CHENGULA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA
MBEYA, BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA. MAREHEMU WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA NI
WANNE AMBAO NI 1. THOMAS SIMFUKWE (35)
2. EXAVERY MUMBISA (34) 3. AMINA MAIKO (30) 4. NEEMA ALMASI 5. HEBELI MKILIMI 6. ROSE HEZRON HALELE NA 7. ALIYEFAHAMIKA KWA JINA
MOJA JANUARI.
HATA HIVYO
MIILI YA MAREHEMU WATATU BADO KUTAMBULIWA. AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU KUMI NA MOJA [11] WALIJERUHIWA AMBAO
MAJERUHI SITA [06] WANAUME, WANNE [04] WANAWAKE, WAWILI WAMELAZWA KATIKA
HOSPITALI YA RUFAA MBEYA AMBAO NI DEREVA AITWAYE JOHN EMMANUEL MZUMBA (36) MKAZI WA MLOWO NA KONDAKTA AITWAYE CHRISTIAN MTENDE (31) MKAZI WA MLOWO NA
WENGINE SABA WALIPELEKWA KATIKA HOSPITALI YA SERIKALI WILAYA YA MBOZI NA KITUO
CHA AFYA TUNDUMA KWA MATIBABU.
CHANZO CHA
AJALI NI UZEMBE WA DEREVA WA TOYOTA COASTER KUTAKA KUYAPITA MAGARI YALIYOKUWA
MBELE YAKE BILA KUCHUKUA TAHADHARI.
KATIKA TUKIO LA PILI:
DEREVA WA LORI
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA HAMAD AHMAD @
MASAWE (30) MKAZI WA DSM AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA GARI ALILOKUWA
AKIENDESHA LENYE NAMBA ZA USAJILI T.769 ARX AINA YA SCANIA KUACHA NJIA NA
KUPINDUKA ENEO LA SENJELE WILAYA YA MBOZI.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 21.12.2014
MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI HUKO
KATIKA KIJIJI CHA SENJELE, KATA YA RUANDA, TARAFA YA IYULA, WILAYA YA MBOZI,
BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI.
MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHUIWA HASPITALI YA SERIKALI YA WILAYA YA MBOZI.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA
SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA.
No comments:
Post a Comment