Katibu
Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Yohana Sefue, amemsimamisha kazi kwa muda
Ndugu Eliakim Maswi, Katibu Mkuu ya Wizara ya Nishati na Madini, ili
kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake, kama ilivyoelekezwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Balozi
Sefue amemsimamisha kazi Ndugu Maswi kuanzia leo, Jumanne, Desemba 23,
2014, kwa kutumia madaraka aliyonayo kama Mamlaka ya Nidhamu kwa
Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu
Taarifa
iliyotolewa na Ofisi ya Balozi Sefue mjini Dar es Salaam imesema kuwa
amechukua hatua hiyo "Kwa mujibu wa Kifungu 4(3) (d) cha Sheria ya
Utumishi wa Umma, Na. 8 ya mwaka 2002 (kama ilivyorekebishwa)" ambapo
"Katibu Mkuu Kiongozi ndiye Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma
wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu."
Badala
yake, Balozi Sefue amesema kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na
Madini, Mhandisi Ngosi C. Mwihava atakaimu nafasi ya Katibu Mkuu, Wizara
ya Nishati na Madini, hadi uchunguzi dhidi ya Ndugu Eliakim C. Maswi
utakapokamilika
No comments:
Post a Comment