Monday, December 22, 2014

MKUU WA CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA (MUST) PROFESA MARK MWANDOSYAAWATUNUKU VYETI WAHITIMU 1068 KATIKA MAHAFALI YA PILI YA CHUO HICHO.

MKUU wa Chuo Kikuu cha Sayansina Teknolojia Mbeya(MUST) Profesa Mark Mwandosya amewatunuku vyeti wahitimu 1068 katika mahafali ya pili ya chuo hicho katika sherehe zilizofanyika katikaUkumbi wa Chuo kilichopo Iyunga jijini Mbeya.






Diana Kaijage mwanafunzi wa mwaka wa tatu kitengo  Laboratory Technology  akimwelezea mkuu wa chuo hicho jinsi wanavyojifunza Mambo ya maabara

John Mogha Mhadhiri Msaidizi  idara ya sayansi na Biashara  akimwelezea Mkuu wa chuo jinsi wanavyowafundisha wanachuo katika idara hiyo

MKUU wa Chuo Kikuu cha Sayansina Teknolojia Mbeya(MUST) Profesa Mark Mwandosya akipata maelezo mafupi toka kwa Rosemary Kavishe Idara ya Usanifu majengo 

MKUU wa Chuo Kikuu cha Sayansina Teknolojia Mbeya(MUST) Profesa Mark Mwandosya akiapata maelezo mafupi toka kwa Mmeneja Mradi wa MCB Lupakisyo Mwalwiba jinsi kitengo chake kinavyofanya kazi chuoni hapo


MKUU wa Chuo Kikuu cha Sayansina Teknolojia Mbeya(MUST) Profesa Mark Mwandosya akipata maelezo toka kwa mwanafunzi wa mwaka idara ya uhandisi umeme Ramadhani Saidi


MKUU wa Chuo Kikuu cha Sayansina Teknolojia Mbeya(MUST) Profesa Mark Mwandosya akipata maelezo toka kwa Peter Shektondo idara ya Computer mwaka wa 3







 Mwenyekiti waBaraza la Chuo, Profesa Penina Mlama akimkaribisha Mkuu wa Chuo cha Sayansi nateknolojia Mbeya, Profesa Mark Mwandosya kuwatunuku vyeti wahitimu.

Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Sayansi naTeknolojia Mbeya(MUST),Profesa Joseph Msambichaka, akisoma Risala yake wakati wamahafali ya Pili ya Chuo hicho, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Chuohicho Profesa Mark Mwandosya(Mb) na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais kazi maalum.




Mshereheshaji wa sherehe hiyo


MKUU wa Chuo Kikuu cha Sayansina Teknolojia Mbeya(MUST) Profesa Mark Mwandosya akipokea zawadi toka kwa Mwenyekiti waBaraza la Chuo, Profesa Penina Mlama 






MKUU wa Chuo Kikuu cha Sayansina Teknolojia Mbeya(MUST) Profesa Mark Mwandosya amewatunuku vyeti wahitimu1068 katika mahafali ya pili ya chuo hicho katika sherehe zilizofanyika katikaUkumbi wa Chuo kilichopo Iyunga jijini Mbeya.
Mbali na Mahafali hayo uongoziwa Chuo hicho umeeleza mikakati yake katika kukabiliana na upungufu wa Walimuwa masomo ya Sayansi katika Shule za Sekondari nchini, kwa kuanzisha kitengocha Elimu ya sayansi.
Hayo yalibainishwa  na Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Sayansi naTeknolojia Mbeya(MUST),Profesa Joseph Msambichaka, katika Risala yake wakati wamahafali ya Pili ya Chuo hicho, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Chuohicho Profesa Mark Mwandosya(Mb) na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais kazi maalum.
Profesa Msambichaka alisemauongozi wa Chuo unaendelea na mikakati na matayarisho ya kuanzisha Chuo chaelimu ya sayansi kwa ajili ya kufundisha walimu wa sayansi watakaofundishashule za Sekondari ili kupunguza changamoto ua upungufu wa walimu wa Sayansinchini.
Alisema mkakati huo unawezekanakutoka na Chuo kufanikiwa  kuanzisha vyuovitatu katika kipindi cha Mwaka mmoja ndani ya Kampasi kuu ya Chuo cha Sayansina Teknolojia Mbeya ambavyo ni Chuo cha Uhandisi na Teknolojia, Taasisi yaSayansi na Teknolojia na Skuli ya mafunzo ya Biashara.
Aidha alitoa wito kwa Wahitimukutumia ujuzi walioupata katika kuchangia kuongeza kasi ya maendeleo ya taifasambamba na kuwa mabalozi wazuri wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya katikakuendeleza matumizi ya sayansi na Teknolojia na hivyo kuleta ufanisi katikashughuli za ujenzi wa taifa.
Kwa upande wake Mwenyekiti waBaraza la Chuo, Profesa Penina Mlama akimkaribisha Mkuu wa Chuo cha Sayansi nateknolojia Mbeya, Profesa Mark Mwandosya kuwatunuku vyeti wahitimu alisemaMahafali hiyo ni ya pili tangu kuanzishwa na kupandishwa hadhi kutoka Taasisiya Sayansi na Teknolojia hadi kuwa Chuo kikuu. Alisema jumla ya wahitimu 1068watatunukiwa vyeti ambapo kati yao wahitimu 821 ni wa ngazi ya Stashahada yakawaida na wahitimu 246 ni wa ngazi ya Shahada ya Kwanza katika fani zaUhandisi wa Kompyuta, Uhandisi wa mitambo, uhandisi ujenzi, uhandisi umeme,usanifu majengo na uongozi wa biashara.
Profesa Mlama aliongeza kuwakatika takwimu za wahitimu mwaka huu zinaonesha kuwa kati ya wahitimu 1068wahitimu wa kike ni 160 sawa na asilimia 15 ikilinganishwa na awamu iliyopitaambayo ilikuwa na asilimia 10 ya wahitimu wa kike hivyo kufanya kuwa naongezeko la udahili wa watoto wa kike kuongezeka kwa asilimia 5.
Alisema pamoja na ongezeko hilobado inatakiwa jitihada za maksudi ili kuongeza udahili wa wanafunzi wa kikekatika Chuo hicho ambapo pia aliupongeza Mfuko wa elimu Tanzania(TEA) kwamchango wao mkubwa wa ruzuku ulivyowawezesha wanafunzi wa kike zaidi kujiungana Chuo hicho.
Mwisho.
Na Mbeya yetu

No comments: