Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Dk.Mighanda Manyahi kuwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO).
Kwa taarifa iliyotolewa leo na kwa vyombo vya habari -na kusainiwa na
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini ilisema ,kufuatia uteuzi
huo,Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter -Muhongo amewateua
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO .Wajumbe wa bodi walioteuliwa ni Kissa Vivian Kilindu,Juma Mkobya,Dk.Haji Semboja,Shabaan Kayungilo,Dk.Mtesigwa Maingu,Bodi Mhegi,Felix Kabodya pamoja na Dk.Nyamajeje Weggoro.
Taarifa hiyo ilisema bodi hiyo imeanza kazi Januari 1 na itaishia Februari 31 Mwaka 2017
chanzo: ikulu
No comments:
Post a Comment