MSAJILI
wa Vyama Vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amevitaka vyama vyote
vya siasa kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria , katiba na kanuni
ili kuepusha migogoro.Aidha msajili huyo amevitaka vyama hivyo mfano
mzuri wa kwa jamii kwa kudumisha amani na utulivu ndani ya vyama vya
siasa.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Msajili huyo katika taarifa yake aliyoitoa kwa
vyombo vya habari kufuatia kuwepo kwa wimbi kubwa la migogoro ndani ya
vyama hivyo. "Endapo kwa bahati mbaya mgogoro ukiibuka, unatakiwa
utatuliwe kwa utaratibu na namna ambayo itadumisha amani na utulivu
ndani ya chama," alisema Jaji Mutungi.
Jaji
Mutungi amewataka wanachama wa kawaida wa vyama vya siasa kupenda amani
na utulivu ndani ya chama na kuepuka migogoro kwa kuheshimu na kufuata
mfumo au taratibu za kuwasilisha malalamiko uliopo ndani ya chama au
taasisi husika. Pia wawe wavumilivu mpaka watakapopata majibu ya
malalamiko yao kutoka katika utaratibu huo uliowekwa na taasisi husika.
Aliongeza
kuwa ofisi yake inajitahidi kuepusha na kutatua migogoro ndani ya vyama
kwa kuchukua hatua zifuatazo, ambazo ni kuvihimiza vyama vya siasa
kuheshimu sheria,kuzingatia misingi ya demokrasia na utawala bora,katiba
na kanuni zake, kusuluhisha mgogoro unapoibuka, "Na hivi sasa
tumewasilisha Serikalini mapendekezo ya marekebisho ya sheria
yatakayosaidia kuepusha migogoro ndani ya vyama," alisisitiza.
Ameiomba
jamii ikemee tabia ya migogoro isiyo na tija ,inapoona vyama vya siasa
havitekelezi wajibu wake, badala yake vinajikita katika migogoro ndani
ya ndani.
No comments:
Post a Comment