Friday, January 9, 2015

“MZEE WA NGUZO ZA UMEME”WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO APATA MAPOKEZI MAKUBWA WILAYANI KISHAPU MKOANI SHINYANGA.

unnamed1Z 
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anna Rose Nyamubi (mbele) akizungumza na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) pamoja na watendaji wake waliomtembelea ofisini kwake kabla ya kuanza ziara rasmi katika mkoa wa Shinyanga. Profesa Muhongo anafanya ziara katika mkoa huo kukagua miradi ya umeme inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili pamoja na kuzungumza na wananchi.
unnamed2Z 
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisalimiana na baadhi ya wakazi wa wilaya ya Kishapu mara baada ya kuwasili wilayani humo. Kushoto ni Mbunge wa Kishapu Suleiman Masoud Nchambi
unnamed3Z 
Wakazi wa Kata ya Bubiki wilayani Kishapu wakimpokea kwa shangwe Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo mara alipowasili wilayani hapo huku wakiwa na mabango yaliyosomeka “ Profesa wa Kweli, Nchi sasa inang’aa vijijini, Wewe ni Jembe”.
unnamed4Z 
Mmoja wa wakinamama kutoka kata ya Igubi wilayani Kishapu mkoani Shinyanga akimfunga vitambaa mkononi Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kama heshima kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kusambaza umeme katika kata hiyo. Kata hiyo ni moja ya kata zinazonufaika na mradi wa umeme vijijini unaotekelezwa na REA Awamu ya Pili
unnamed5Z 
Mbunge wa Kishapu Suleiman Masoud Nchambi (katikati) akijumuika na wakazi wa Kata ya Igumbi iliyopo wilayani Kishapu kucheza ngoma ya kumpongeza Waziri wa Nishati na Madini kwa juhudi zake za kusambaza umeme katika kata hiyo pamoja na jimbo lake.
unnamed6Z 
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) na Mbunge wa Kishapu Suleiman Masoud Nchambi (kulia) wakifuatilia taarifa ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini inayosimamiwa na REA Awamu ya Pili iliyokuwa inatolewa na Meneja Utaalamu Elekezi kutoka REA Gissima Nyamohanga (hayupo pichani)
unnamed7Z 
Mtaalamu kutoka kampuni ya kusambaza umeme vijijini ya LTL (PVT) LTD Michael Marenye (kushoto) akitoa taarifa ya hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa miundombinu ya umeme katika wilaya ya KIshapu. Kulia ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.
unnamed8Z 
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na wakazi wa Kata ya Mwamalasa wilayani Kishapu.
unnamed10Z 
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Suleiman Masoud Nchambi akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo
Wakazi wa Bubiki wilayani Kishapu wakimkabidhi Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) zawadi ya mbuzi wawili kama pongezi kwa kazi nzuri ya kusambaza umeme katika kata hiyo. unnamed12Z 
Sehemu ya umati wa watu kutoka Kata ya Bubiki wakishangilia hotuba ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani).

No comments: