Monday, January 12, 2015

Rais Kikwete katika Sherehe za Miaka 51 ya mapinduzi Zanzibar

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh.Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na Rais Mstaafu Mh Benjamin Mkapa wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 51 ya  Mapinduzi  Zanzibar zilizofanyika kwenye uwanja wa Amani, Katikati ni mama Fatma Karume na Waziri Mkuu mstaafu Salim Ahmed Salim (Picha na Freddy Maro wa Ikulu) unnamed2 
Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia Mkono wananchi wakati alipowasili katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika kilele cha Sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyofanyika leo,[Picha na Ikulu.} unnamed2h 
Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama leo wakati wa  Sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar akifuatana na Paredi Kamanda Luteni kanali Mohamed Khamis Adam  katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja ,[Picha na Ikulu.} unnamed4h 
Wananchi mbali mbali waliohudhuria katika sherehe za kilele cha miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar wakimasikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake leo katika kilele hicho Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.} unnamed7h 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika leo katikauwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.}

No comments: