Tuesday, January 27, 2015

WIZARA INAYOSIMAMIA VIJANA NA HARAKATI KUWAKOMBOA VIJANA WA RUNGWE MKOANI MBEYA

1
Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa wa pili kushoto akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Eng. Harold D. Sawaki katikati walipofika Wilaya ya Rungwe jana kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana wa Wilaya hiyo. Kulia ni Afisa Maendeleo ya Jamii Bw. Ason Nzowa, wa pili kulia ni Afisa Michezo na Vijana Mkoa wa Mbeya Bw. George Mbijima na wa kwanza kushoto ni Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga.
2
Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga kulia akizungumza na vijana wa Wilaya ya Rungwe wakati wa semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana jana karika Wilaya ya Rungwe. Katikati ni Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa na kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele.
3
Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele akitoa mada wakati wa semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana jana karika Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya.
4
Kijana Daudi Essau Seme kutoka katika kikundi cha Tukuyu Bodaboda Saccoss Limited akichangia wakati wa semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana jana karika Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya.
5
Baadhi ya vijana wa Wilaya ya Rungwe katika kikundi wakijadiliana namna ya kuandika andiko la mradi baada ya kuelimishwa wakati wa semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana jana katika Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya.
7
Maafisa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakimsikiliza kwa makini kijana Boniel Soka (kushoto) kutoka kikundi cha Muungano Makandana kinachojishughulisha na upandaji miti ya aina mbalimbali wakati wa ziara ya kukagua miradi ya vijana wa Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya.
by SOLO Mazalla 
KINGOTANZANIA
Post a Comment