WAKLIMA NA WANUNUZI WA MAZAO YA CHAKULA WAKIWA KATIKA SOKO LA TANDALE WILAYANI RUNGWE |
MKULIMA AKIFIKA KUUZA MKUNGU WA NDIZI AMBAO KWA SASA MKUNGU KAMA HUO UNAUZWA SHILINGI ELFU MBILI |
NDIZI ZIKIWA ZIMEKOSA WANUNUZI KATIKA SOKO LA TANDALE TUKUYU NA HII INATOKANA KUWA HUU NI MSIMU WA ZAO LA NDIZI HIVYO BEI YA NDIZI HUYUSHA SANA NA WAKULIMA KUUZA KWA BEI YA CHINI BILA YA KUPATA FAIDA |
MMOJA WA WANUNUZI WA ZAO LA MAPARACHICHI KATIKA SOKO LA TANDALE |
Soko kuu la wakulimaTandale
mjini Tukuyu Wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya limekosa wateja wa mazao ya chakula
na kusababisha kushuka kwa bei ya mazao hayo hasa mazao ya ndizi mbalimbali
maparachichi na mazao ya mbogamboga
ambayo ndio hutegemea kwa wingi na
wateja wanao toka mikoa ya jirani
Wakizungumza sokoni hapo wakulima na wanunuzi wa mazao ya
chakula wamesema kwamba gulio la kipindi hiki wateja wamekuwa wachache
ukilinganisha na vipindi vingine na bei ya mazao hutegemeana na wateja
waliofika siku hiyo ya gulio hivyo kipindi hiki wakulima hulazimika kuuza kwa
bei ya hasara kufuatana na bei anayoitaka mnunuaji kwa kuogopa kubakiwa na mzigo mkubwa ambapo kwa
sasa mkungu mzuri wa ndizi katika soko
la Tandale unafikia shilingi elfu tatu.
“Kipindi hiki bei imeshuka kabisa na kumumiza mkulima wa
mazao ya chakula hasa zao la ndizi na
maparachichi ndiyo yamekuwa na bei ya chini sana kwani mkungu mkubwa moja wa ndizi aina ya mzuzu unauzwa kwa
shilingi elfu nne kwa elfu tatu na ndizi aina ya malindi na aina zingine
zinauzwa kwa shilingi elfu moja mia tano kwa elfu moja kwa mkungu uliokomaa
vizuri na mkubwa na kwa upande wa maparachichi ujazo wa gunia moja limeuzwa kwa
shilingi elfu ishirini na tano, wakati kipindi kukiwa na wateja wengi ndizi huuzwa kwa bie ya shilingi elfu nane
kwa elfu saba kwa aina ya mzuzu na elfu nne kwa elfu tatu mia tano kwa aina nyingine za ndizi na gunia la
maparachichi huuzwa kwa shilingi elfu thelathini hadi elfu Alobaini.
Bei ya jumla kwa
mazao ya chakula katika soko la tandale mjini Tukuyu gunia la mahindi limeuzwa kwa bie ya shilingi
elfu therathini, viazi mviringo ujazo wa gunia vimeuzwa kwa shilingi elfu
sitini na gunia la maparachichi limeuzwa kwa shilingi elfu ishirini na tano
huku ndizi mkungu moja mkubwa umeuzwa kwa shilingi elfu nne kwa elfu tatu kwa
aina ya mzuzu na elfu moja kwa aina ya malindi.
TUMAIN OBEL
KINGO TANZANIA
No comments:
Post a Comment