Katibu
Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kushoto) akitoa
maelezo ya kumkaribisha Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na
Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu (Kulia) wakati alipofanya ziara ya
kujitambulisha kwa Tume ya Mipango.
Waziri
wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu
(Wapili kushoto) akizungumza na baadhi ya watendaji wa Ofisi ya Rais,
Tume ya Mipango alipotembelea na kujitambulisha Tume ya Mipango.
Wanaomsikiliza ni Katibu Mtendaji, Dkt. Philip Mpango (Kushoto), Naibu
Katibu Mtendaji (Miundombinu na Huduma), Mhandisi Happiness Mgalula
(Wapili kulia) na Naibu Katibu Mtendaji (Biashara za Kimataifa na ya
Kiuchumi), Bw. Paul Sangawe (Kulia).
Baadhi
ya watumishi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakimsikiliza Waziri wa
nchi (Ofisi ya Rais) na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu (Hayupo pichani)
alipotembelea na kujitambulisha Tume ya Mipango. Mwenyekiti
wa Chama cha Wafanyakazi (TUGHE) Tawi la Mipango, Bw. Stephen Katemba
(aliyesimama) akizungumza wakati Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais)
Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu alipofanya ziara ya
kujitambulisha kwa Tume ya Mipango.
Katibu
Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kushoto) akimkabidhi
zawadi za vitendea kazi Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na
Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu alipofanya ziara ya kujitambulisha kwa Tume
ya Mipango.
Naibu
Katibu Mtendaji (Miundombinu na Huduma), Mhandisi Happiness Mgalula
(Kushoto) akimkabidhi zawadi Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na
Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu alipofanya ziara ya kujitambulisha kwa
Tume ya Mipango.
…………………………………………………………………
Na Saidi Mkabakuli
Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais)
Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu amefanya ziara ya
kujitambulisha kwa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ambayo ni moja taasisi
anazoziratibu.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo
Dkt. Nagu alitoa wito kwa Tume ya Mipango ijielekeze katika kujibu
changamoto kuu za kiuchumi zinazowakabili watanzania kwa sasa ikiwemo
umaskini miongoni kwa Watanzania walioko vijijini, ukosefu wa wa
viwanda vya kuongeza thamani mazao hasa kipindi hiki Tanzania
inapoelekea kwenye uchumi wa gesi.
Dkt. Nagu aliasa Tume ya Mipango kufanya tafiti mbalimbali za kiuchumi na kijamii zitakazotoa majibu ya changamoto hizo.
“Kwa kuwa moja ya majukumu ya Tume
ya Mipango ni kuandaa mipango ya maendeleo ya muda mrefu, kati na ile
ya kila mwaka na pia kufanya tafiti mbalimbali za kiuchumi na kijamii,
napenda kusisitiza kuwa mipango inayoandaliwa ijielekeze katika kujibu
changamoto hizo kubwa zinazowakabili wananchi wetu ili kuhakikisha kuwa
tunafikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025,” alisema Dkt.
Nagu.
Kwa mujibu wa malengo makuu ya
Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, serikali imejipanga kuhakikisha maisha
bora na mazuri kwa kila mtanzania, utawala bora unaozingatia sheria, na
kujenga uchumi imara, wa kisasa na ushindani.
Akizungumza wakati wa kumkaribisha
Dkt. Nagu, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango
alisema kuwa majukumu ya msingi ya Tume ya Mipango ni kutoa dira na
mwongozo wa uchumi wa Taifa pamoja na kubuni sera za uchumi na mikakati
ya mipango ya maendeleo ya Taifa; usimamizi wa uchumi na kufanya utafiti
katika nyanja za uchumi na maendeleo ya jamii.
Dkt. Mpango aliongeza kuwa kwa
sasa Tume ya Mipango inafanya kazi ya kuratibu utekelezaji wa Mpango wa
Maendeleo wa Taifa 2014/15 pamoja na uandaaji wa Mpango wa Maendeleo wa
Taifa 2015/16 na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2016/17.
“Vilevile, Tume ya Mipango
tumejidhatiti katika kuandaa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano
2016/17 – 2020/21 ambao utajikita katika kuifikisha tanzania kuwa ni
nchi ya viwanda,” alisema Dkt. Mpango.
Kwa mujibu wa Dkt. Mpango, tangu
kuundwa upya kwa Tume ya Mipango mwaka 2008, imefanikiwa kukamilisha
kazi kubwa za kitaifa ikiwemo kufanya mapitio ya Dira ya Taifa ya
Maendeleo 2025, kuandaa Mpango Elekezi wa Miaka 15 (2011/12 – 2025/26
pamoja na kuandaa Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12
– 2015/16) na kuratibu utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Idadi ya Watu
2006.
Kazi nyingine ni pamoja na kuandaa
Mipango ya Maendeleo ya Taifa kila Mwaka, kuandaa mfumo wa ufuatiliaji
na utekelezaji wa miradi ya Matokeo Makubwa Sasa na kuratibu uanzishwaji
wa President Delivery Bureau (PDB), Kuandaa Mwongozo wa
Usimamizi wa Uwekezaji katika Sekta ya Umma (Public Investiment
Management – Operational Manual – PIM-OM), na kufanya tafiti mbalimbali
za kiuchumi na kijamii.
No comments:
Post a Comment