Sunday, February 15, 2015

KAMPUNI YA OFF GRID ELETRIC KUFUNGA UMEME WA SOLA NYUMBA MILIONI MOJA NCHINI

 Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA), Lutengano Mwakahesya (PhD) (kushoto), pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Off Grid Electric Ltd, wakionesha seti ya mfumo wa vifaa vya umeme wa sola ambavyo vitatumika katika mpango wa kutumia umeme wa sola kwa nyumba milioni 1 wakati wakiwaonesha waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi.
  Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA), Lutengano Mwakahesya (PhD) (kulia), pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Off Grid Electric Ltd, Erica Mackey wakiteta jambo wakati wa mkutan huo na waandishi wa habari.
 Meneja wa Miradi Maalumu wa Kampuni hiyo, James Sawabini (kulia), akiandaa vifaa hivyo kabla wakati vikioneshwa kwa waandishi wa habari.
 Wapiga picha kutoka vyombo mbalimbali vya nahabri 
wakichukua taarifa hiyo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
………………………………………………………………….
Dotto Mwaibale
 
SERIKALI ya Tanzania imesema hadi ifikapo mwaka 2017, itakuwa imetimiza mpango mahususi wa kutumia umeme wa sola uitwao ‘One Solar Homes’ katika nyumba milioni moja.
 
Akizungumza Dar es Salaam leo mchana , Mkurugenzi Mkuu wakala wa Nishati Vijijini, Lutengano Mwakahesya, alisema mradi huo unatarajia kutoa huduma ya umeme kwa asilimia 10 ya watu nchini na ajira 15000 zitakazohusu sola.
“Kwa hali ya sasa asilimia 86 ya watanzania wanategemea mafuta ya taa na mishumaa kwa ajili ya kupata mwanga zana ambazo zina madhara kwa afya, mazingira na isiyotoa matokeo ya kutegemewa,” alisema.
 
Alisema mpango huo ni mfano mzuri kwa mataifa mengine ambayo yana malengo sambamba na mradi wa Power Afrika Initiative uliotangazwa na Rais wa Marekani Barack Obama mwaka 2013, wenye malengo ya kufikisha umeme kwa nyumba milioni 60 barani Afrika.
 
Mwakahesya alisema mpango huo utaendeshwa na kampuni ya Off Grid Electric Ltd, kampuni ya sola inayokuwa kwa kasi kwa nchi zinazoendelea, huku Tanzania ikijulikana kwa jina la ‘M-POWER’.
Alisema malipo ya mwezi ni madogo kwa kiasi cha senti 20 za 
kimarekani kwa siku ambayo ni sawa na sh. 360 ya kitanzania.
“Watanzania watafaidika na mpango huu utakaowafikishia umeme 
mzuri na wenye uhakika kwa ushirikiano na Off Grid Electric Ltd inchi yetu inaweza ikaongoza katika mradi wa dunia wa nishati ifikapo mwaka 2030,” alisema.
 
Alisema mradi huo utatumia fedha za kimaendeleo na mtaji binafsi dola milioni 10, kama uwekezaji nchini Tanzania, ikitangazwa mapema mwaka huu shirika la kimataifa la fedha litatoa kiasi cha dola za Marekani milioni saba katika hatua ya kwanza ya mradi.

No comments: