Monday, February 23, 2015

NECTA yafanikiwa kudhibiti wizi na udanganyifu katika mitihani

NEC1 
Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Daniel Mafie akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya baraza hilo kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam

NEC2 
Msaidizi wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Glee Magembe, akieleza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam leo.Kushoto kwake ni Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa baraza hilo, Daniel Mafie.
NEC3 
Msaidizi wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Glee Magembe, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya baraza hilo kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam leo.Kushoto kwake ni Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa Baraza, Daniel Mafie, Afisa Habari wa MAELEZO, Frank Mvungi na Afisa Habari wa NECTA, John Nchimbi.
NEC4 
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria kwenye mkutano kati ya Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam
………………………………………………………………
Frank Mvungi-Maelezo
BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA) kwa kushirikiana na Kamati za Uendeshaji Mitihani za mikoa na wialaya limefanikiwa kudhibiti na kuondoa tatizo la wizi wa mitihani katika mitihani ya Taifa.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa Idara ya Utawala na Fedha wa NECTA, Daniel Mafie wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliolenga kueleza mafanikio yaliyofikiwa na Baraza hilo.

Mafie amesema pamoja na kudhibiti wizi huo, pia NECTA limefanikiwa pia kudhibirti udanganyifu wakai wa ufanyaji wa mitihani ya Taifa.
Alisema katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi udanganyifu umepungua kutoka watahiniwa 9,736 mwaka (2011) hadi 293 mwaka 2012.

Kwa Mwaka 2013 udanganyifu umepungua kutoka watahiniwa 13 hadi 01 mwaka 2014 hali inayoonyesha kuwa tatizo hilo limedhibitiwa kwa kiasi kikubwa.
“Katika mtihani wa kidato cha nne (CSEE) udanganyifu umepungua kutoka watahiniwa 3,303 (2011), hadi 789 mwaka 2012” alisema Mafie.

Aidha katika Mtihani wa kidato cha Sita (ACSEE)Mafie alibainisha kuwa udanganyifu umepungua kutoka watahiniwa 11 mwaka 2011 hadi 6 mwaka 2012,wakati mwaka 2013 watahiniwa waliofanya udanganyifu walikuwa 4 na kupungua hadi 3 mwaka 2014.
Katika kuboresha huduma zinazotolewa na NECTA, Mafie alibainisha kuwa Baraza hilo limeanzisha utaratibu wa kutoa matokeo ya mitihani kwa njia ya mtandao wa simu ambapo unatakiwa kutuma ujumbe mfupi wa maneo (SMS) ambao ni gharama nafuu.
Ujumbe huo unatumwa kwenda namba 15311 ambapo mtahiniwa anatuma neno Matokeo* namba ya shule/kituo*namba ya mtahiniwa*aina ya mtihani *mwaka mtihani ulipofanyika, na baada ya hapo atapokea matokea yake.

Alisema kujua nafasi ya shule Kitaifa,Mkoa,Halmashauri andika neon rank * namba ya shule/kituo* aina ya mtihani* na mwaka mtihani ulipofanyika.
Suala la wizi wa mitihani ya Taifa na udanganyifu katika mitihani hiyo, limekuwa moja ya mambo yanayolikabili baraza hilo katika miaka ya hivi karibuni.

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) ni Taasisi ya Umma chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iliyoanzishwa kwa ajili ya kuendesha Mitihani ya Taifa.
NECTA ilianzishwa kwa sheria ya Bunge Na.21 ya mwaka 1973 na marekebisho yake ya mwaka 1998 na 2002.

No comments: