Thursday, February 12, 2015

NGASSA ACHANGIWE?

Mshambuliaji wa Yanga Mrisho Ngassa amekiri kwamba yupo hoi kiuchumi. Mshahara wake wote wa mwezi unaishia kulipa deni linalotokana na kuvunja mkataba wake Azam ili arudi Yanga huku msemaji wa Wanajangwani, Jerry Muro, akisema hawawezi kumlipia deni hilo bila makubaliano kwani timu ni ya wanachama. Je, ni wakati kwa wafurukutwa na wanachama wa Yanga kumnusuru Ngassa kwa kumchangia ili amalize deni lake mapema?
Chanzo:Mwanaspoti
Post a Comment