Wasichana wa shule waliotekwa nyara na Boko Haram
Rais
anayeondoka mamlakani nchini Nigeria Goodluck Jonathan, amesema
amesikitishwa kuwa siasa zilipewa kipau mbele, kuliko maslahi ya
wasichana waliotekwa nyara na kundi la Boko Haram kutoka shule moja
kwenye mji wa Chibok katika jimbo la Borno.
Rais
Jonathan, ambaye alishindwa kwenye uchaguzi wiki mbili zilizopita
anasema kuwa bado ana uhakika kuwa wasichana hao waliotekwa nyara mwaka
mmoja uliopita watapatikana wakiwa salama
Msemaji
wa kundi linalojiita Bring Back Our Girls (Aisha Yesufu) aliiambia BBC
kuwa serikali ya rais Jonathan kwanza haikuamini kuwa wasichana hao
walikuwa wametekwa.
Lakini
rais Jonathan alikilaumu chama cha upinzai kinachosimamia jimbo na Borno
kwa kusababisha mchanganyiko wakati wasichana hao walipotekwa.
Siku ya
Jumatatu mkazi mmoja wa mji ulio kaskazini mashariki mwa nchi wa Gwoza
alisema kuwa aliwaona baadhi ya wasichana hao wiki tatu zilizopita
walipokuwa wakitoka kwenye nyumba moja kubwa karibu na nyumba yake.CHANZO:BBC (Muro)
No comments:
Post a Comment