Kundi
la Watanzania 26 limerejea nyumbani kutoka Afrika Kusini leo tarehe 26
Aprili, 2015 kufuatia mashambulizi ya wazawa dhidi ya wageni. Kundi hilo
la kwanza kurejea nyumbani liliwasili katika Uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere saa 11 alfajiri na Ndege ya Fast
Jet.
Watanzania hao walikuwa wanaishi
katika kambi za dharura za Isipingo na Phoenix zilizopo jijini Durban.
Walisindikizwa kurudi nyumbani na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania
nchini Afrika Kusini, Bw. Elibahati Lowassa. Zoezi la kuwarejesha
wananchi hao lilisimamiwa na kuratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini
Afrika Kusini.
Wakati huo huo, Ubalozi wa
Tanzania nchini Afrika Kusini umepata taarifa kuwa kuna Watanzania
wengine wapatao 20 wanaishi kwenye Kambi ya Hillbrough jijini
Johannesburg. Ubalozi umetuma Afisa kwenda katika kambi hiyo ili kufanya
uhakiki wa taarifa hizo kwa madhumuni ya kuwarejesha nyumbani Tanzania
haraka iwezekanavyo.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
25 Aprili 2015
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
25 Aprili 2015
No comments:
Post a Comment