Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha ishara mbalimbali kwa
msisitizo wakati akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye mji mdogo wa Katoro jimbo la Busanda mkoani Geita
wakati Katibu mkuu huyo akiendelea na ziara yake mkoani humo, Kinana
anafanya ziara mkoani Geita yenye lengo la kukagua na kuhimiza
utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010-2015
inayotekelezwa na serikali huku akihimiza uhai wa Chama cha Mapinduzi
CCM, Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
CCM.
Katika
mkutano huo Kinana amewaambia wananchi hasa wachimbaji wadogowadogo wa
Nyarugusu kwamba hataki kuwa mmoja wa wanaotoa ahadi bila kutekelezeka
na hataki kuahidi uongo, Mimi ninalichukua hili ili nikalifanyie kazi na
nitarrudi hapa Katoro kuwapa jibu kama nimefanikiwa au sijafanikiwa.
Lakini
nilichoambiwa ni kwamba Rais ameshabariki ili wachimbaji wadogo wapewe
eneo fulani hapo Nyarugusu ili waendelee kuchimba na kujipatia riziki
yao, Lakini jambo la kushangaza ni kwamba amri ya Rais haijatekelezwa
yaani watendaji wamemwangusha Rais kwa madai kwamba Shirika la madini la
serikali la STAMICO na kampuni ya madini ya TANZAM bado hawajaafikiana
kisheria ili kuachia eneo hilo la Nyarugusu ili wachimbaji wadogo
kukabidhiwa kwa ajili ya kuendeleza uchimbaji ili kujipatia riziki yao.
“Serikali
hii ni ya CCM na inatakiwa kuwasaidia watanzania masikini. Lakini
inashangaza kuona watendaji wa serikali wanachelewa sana kuchukua hatua
na kushughulikia matatizo ya wananchi jambo ambalo linazua malalamiko
kwa wananchi, Niachieni hili ninalichukua na sitaki kuahidi lolote ila
nitarudi na majibu baada ya mwezi mmoja na nina imani litakwisha na
kupata suluhisho la kudumu”.
(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA
FULLSHANGWE-BUSANDA-GEITA)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo katika mkutano huo.
Umati wa wananchi ukiwa umefurika katika mkutano huo ambao umefanyika kwenye mji mdogo wa Katoro mkoani Geita.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye akiwahutubia wananchi katika
mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji mdogo wa Katoro mkoani Geita.
Nape
Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akisisitiza jambo wakati
alipokuwa akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
Katoro.
Mbunge wa jimbo la Busanda Mh. Rolensia Bukwimba akiwahutubia wapiga kura wake wakati mkutano huo ukiendelea.
Mh.Vick Kamata Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Geita akiwasalimia wananchi katika mkutano huo.
Baadhi ya wananchi waliofurika ili kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu
wa CCM mkoa wa Geita Ndugu Gustav Muba akimkaribisha Ndugu Nape Nnauye
hayupo pichani ili apande jukwaani na kuzungumza na wananchi wa
Katoro.
Mkuu
wa wilaya ya Nyang’hwale na kaimu Mkuu wa mkoa wa Geita Ndugu Ibrahim
Nyankanga Marwa akiwasalimia wananchi katika mkutano huo.
Wananchi wakimsubiri Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ili awahutubie.
Baadhi ya wachimbaji madini wadogo wadogo wakimsikiliza Ndugu Kinana
Mmoja
wa wachimbaji wadogo akiwa ambaye jina lake halikfahamika akiwa
ameshikilia kifaa chake cha kazi akifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipkuwa akizungumza nao.
Selemani Magesa na Diwani wa Kata ya Nyarugusu akitoa maelezo ya mgogoro huo mbele ya Kinana.
Baadhi
ya wachimbaji wadogo wakiwa katika mkutano huo wakati Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipowatembelea huko Nyarugusu.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Geita Mh. Vick Kamata akiwasalimia wananchi katika kijiji cha Chikobe mkoani Geita.
Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi wakati alipowatembelea katika kijiji cha Chikobe.
Kutoka
kulia ni Manzie Mangochie Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mkuu wa wilaya ya
Nyang’hwale Ndugu Ibrahim Marwa, Mbunge wa viti maalum mkoa wa Geita Mh.
Vick Kamata na Mbunge wa jimbo la Busana Mh. Rolensia Bukwimba wakiwa
katika picha ya pamoja.
Katibu
mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wakati
alipfanya ziara katika kijiji cha Inyala na kushiriki katika ujenzi wa
zahanati ya kijiji hicho.
Katibu
mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupiga lipu katika
ukuta wa zahanati ya kijiji cha Inyala jimbo la Busanda.
Katibu
mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika kazi ya kulima
barabara ya kijiji cha Nyankanga pamoja na wananchi.
No comments:
Post a Comment