Mwenyekiti wa Chama cha Msalaba mwekundu (Redcross) Mkoa wa Mbeya, Ulimboka Mwakilili, akifungua mafunzo ya Redcross kwa Viongozi wa vyama vya siasa Mkoa wa Mbeya. |
Meneja wa Idara ya Habari na Uhamasishaji wa Redcross Makao makuu, Stellah Marealle akizungumza na washiriki wa Semina ya Redcross kwa viongozi wa vyama vya siasa Mkoa wa Mbeya |
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mikoa na Matawi Redcross makao makuu, Julius Kejo, akitoa mada kwa viongozi wa vyama vya siasa Mkoa wa Mbeya katika mafunzo yaliyotolewa na Chama cha Msalaba mwekundu |
Mratibu wa Chama cha Msalaba mwekundu Zanzibar, Ubwa Suleiman akiwasilisha mada katika mafunzo ya Redcross kwa viongozi wa vyama vya siasa Mkoa wa Mbeya |
Baadhi ya viongozi wa Vyama vya Siasa Mkoa wa Mbeya wakifuatilia mafunzo kuhusiana na Chama cha Msalaba mwekundu |
Mwenyekiti wa Chama cha SAU, Charles Mwampagama akishukuru kwa niaba ya washiriki wengine |
Washiriki wa mafunzo wakifuatilia mada zinazowasilishwa. |
VIONGOZI wa Vyama vya Siasa
mkoani Mbeya wamepatiwa mafunzo na Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania katika
mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Mbeya Paradise Soweto jijini
Mbeya.
Akifungua mafunzo kwa viongozi hao, Mwenyekiti wa Redcross Mkoa
wa Mbeya, Ulimboka Mwakilili, alisema lengo la mafunzo hayo ni kutoa elimu juu
ya historia ya Msalaba mwekundu pamoja na shughuli zake ili ziweze kufahamika
kwa viongozi wa vyama vya siasa.
Mwakilili alisema madhumuni
makubwa ya Chama cha Msalaba mwekundu duniani ni kusaidia wenye dhiki na mateso
na kazi yake kubwa ni kuokoa binadamu wanaopatwa na maafa yanayotokana na
majanga mbali mbali yakilenga kutekeleza kanuni 7 za msingi za Redcross.
Alivitaja vyama vya siasa
vilivyohudhuria mafunzo hayo kuwa ni pamoja na Chama cha Mapinduzi(CCM), Chama
cha Wananchi(CUF),SAU,Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA),UPDP,TADEA,DP
na APPT- Maendeleo.
Kwa upande wake Afisa mahusiano
wa Kamati ya Msalaba mwekundu duniani(ICRC) kutoka Nairobi nchini Kenya,
Viginia Njiru ambaye alitoa historia ya Msalaba mwekundu uanzishaji wake pamoja
na matumizi ya nembo za Redcross.
Aidha alitoa wito kwa watu
mbali mbali kutumia nembo za Redcross kinyume cha sheria kwa madai kuwa baadhi
yao wamekuwa wakitumia kwenye maduka ya madawa, magari ya kubebea wagonjwa na
kwenye mabucha ya nyama jambo alilodai ni kinyume cha utaratibu na kuongeza
kuwa wakibainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment