Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania - TFF, Jamal Malinzi leo ameagana
rasmi na aliyekua kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)
inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, mholanzi Mart Nooij.
Akiongea
na waandishi wa habari leo katika hoteli ya Tansoma, Malinzi amesema
wameamua kuagana nae mbele ya vyombo ya habari kama iliyofanyika pia
wakati wa utambulisho wake wakati wa kuanza kazi.
“Mpira wa
miguu unachangamoto nyingi, watanzania tunasafari ndefu katika
mafanikio ndio maana TFF imeanza kuwekeza katika soka la vijana, sababu
ndio msingi wa kuwa na timu bora ya Taifa” alisema Malinzi.
Duniani
kote chimbuko la timu bora ni soka la vijana na watoto, tukiwa na vijana
wengi walioanza kucheza mpira katika umri mdogo wanapofikia umri wa
kuchezea timu ya Taifa tutakua na kikosi bora.
Nchi za
wenzetu inapofikia kocha kuita wachezaji wa timu ya Taifa anakuwa na
wigo mpana, kwetu sisi wachezaji wanocheza soka nje ya nchi
wanahesabika, hivyo ni lazima tuanze kuwekeza kwenye soka la vijana
TFF
ilishaanza mkakati huo ndio maana kuna timu za U13, U15 ambazo zitakua
zikiingia kambini na kucheza michezo ya kirafiki ndani ya nje kwa lengo
la kupata uzoefu kabla ya kushiriki kuwania kufuzu kwa fainali za vijana
mwaka 2016.
Kikosi
cha U15 kinatarajiwa kufanya ziara mwezi Disemba mwaka huu katika nchi
za Malawi, Zambia, Zimbambwe, Botswana na Afrika Kusini, kisha mwakani
mwezi April 2016 kitaenda Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya kucheza
michezo ya kirafiki.
Naye Mart
Nooij aliyekua kocha wa Taifa Stars, akiongea na waaandishi wa habari
alisema anawashukuru watanzania wote, serikali, wadau wa mpira wa miguu
nchini na TFF kwa sapoti waliyompatia wakati akiwa kocha mkuu wa timu ya
Taifa.
Nooij
alisema alifurahia maisha yake akiwa Tanzania kwa kipindi chote
alichokua akifundisha timu ya Taifa, lakini kwa sababu imefikia mwisho
wa ajira yake hana jinsi anaondoka, lakini ataendelea kuikumbuka
Tanzania na watanzania wote kila siku kwa ukarimu wao.
Wakati
huo huo Rais wa TFF. Jamal Malinzi amemtangaza Charles Mkwasa kuwa kocha
mpya wa Taifa Stars akisaidiwa na kocha Hemed Morocco, Mkwasa ambaye ni
kocha wa Yanga na Morocco kocha wa Mafunzo watafanya kazi kwa kipindi
cha miezi mitatu ambayo timu ya taifa itakua na michezo ya kuwania
kufuzu kwa CHAN na AFCON.
Malinzi
amesema uteuzi wa makocha hao wazawa umezingatia vigezo vya makocha wa
timu ya Taifa kuwa na leseni A ya ukocha kutoka CAF au zinazofanana
kutoka mashiriksho mengine duniani wanaozifanyia kazi, jambo ambalo
makocha hao wazawa wamekizi.
Kocha
Mkwasa atakua akipewa hudumu zote na masilahi (zikiwemo posho) alizokuwa
anapewa kocha aliyeondoka, pia amepewa nafasi ya kuchagua benchi lake
la ufundi la kufanya nalo kazi, hivyo nawaomba wadau wa mpira wa miguu
na watanzania kwa ujumla tuwape sapoti makocha hao wazawa” aliongeza
Malinzi”
Aidha
Kamati ya utendaji ya TFF Iimemteua Alhaj Ahmed Mgoyi kuwa mratibu wa
timu ya Taifa, lengo la uteuzi huo wa Mgoyi ni kuwa kiunganishi kati ya
kamati ya Utendaji na timu ya Taifa.(Muro)
No comments:
Post a Comment