Monday, June 15, 2015

WIZARA YA HABARI VIJANA UTAMADUNI NA MICHEZO YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Shaaban Issa Bin Simba.

ShekheMkuu 
Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Shaaban Issa Bin Simba.
Enzi za uhai wake.
………………………………………………….
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA HABARI VIJANA UTAMADUNI NA MICHEZO
index
Taarifa kwa vyombo vya habari
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara (Mb.) ametuma salamu za rambirambi kwa Baraza Kuu la Waislamu Nchini (BAKWATA) na Waislamu wote nchini kufuatia kifo cha Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Shaaban Issa Bin Simba kilichotokea Jumatatu, tarehe Juni 15,2015 katika hospitali ya TMJ Jijini Dar es Salaam alipokuwa anatibiwa.
Katika salamu hizo, Mhe. Mukangara amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kumpoteza kiongozi huyo ambaye bado Taifa lilikuwa likimuhitaji hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu.
Waziri huyo ameongeza kuwa Mufti atakumbukwa kwa upole , unyenyekevu wake na kutopenda makuu,wakati wa uhai wake marehemu alikuwa tayari kumsikiliza kila mtu bila kujali dini au kabila lake.
“Nimepokea kwa huzuni nyingi taarifa ya kifo cha Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Shaaban Issa Bin Simba ambaye alikuwa Kiongozi anayeshirikiana vizuri na viongozi wote wa serikali na vyama mbalimbali katika kuhakikisha Watanzania wanaendelea kuwa wamoja” amesema .
Amesema Waziri Mukangara: “Nakutumia salamu zangu za rambirambi wewe Katibu Mkuu, BAKWATA na waislamu wote nchini na naungana nanyi katika kuomboleza msiba huu mkubwa katika nchi yetu.
Aidha, kupitia BAKWATA, natuma salamu za dhati ya moyo wangu kwa familia ya marehemu kwa kumpoteza mpendwa wao. Napenda wajue kuwa msiba wao ni msiba wangu. Pia, naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aiweke pema peponi roho ya marehemu … Amina.”
Imetolewa na;
Idara ya Habari(MAELEZO)
15 Juni,2015

No comments: