Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli
akiwahutubia wananchi wa mji wa Tarime katika mkutano wa hadhara wa
Kampeni uliofanyika mjini Tarime leo ambapo Dr. Magufuli amewaomba
wananchi hao kumpigia kura za ndiyo ili aweze kuingia ikulu na
kuwatumikia watanzania kwa ajili ya kuleta mabadiliko bora kwa
watanzania na siyo bora mabadiliko
Naye
Mwigulu Nchemba ambaye ni Mjumbe wa kamati ya Ushindi ya Chama cha
Mapinduzi ameendelea kuwaelimisha Watanzania namna UKAWA wanavyopotosha
Umma kuhusu Kauli za Baba wa Taifa. Nanukuu”Ni kweli Baba wa Taifa
Mwl.Nyerere alisema Watanzania wasipoyapata Mabadiliko ndani ya CCM
watayatafuta NJE ya CCM.”
Kauli
hiyo ya Kutafuta Mabadiliko nje ya CCM ambayo ilisemwa na Baba wa Taifa
ilijikita kwenye Mambo makuu 4 ambayo Watanzania wasipoyaona ndani ya
CCM watakwenda kuyatafuta nje ya CCM.
Jambo la kwanza ni RUSHWA,Mwl.Nyerere
alisema,Watanzania wanahitaji kiongozi anayeweza kukemea Rushwa bila
kuona aibu,Rais aweze kuwambia Jamaa zake kuwa Rushwa ni hatari kwa
Ustawi wa Taifa letu.Hivyo Watanzania wasipopata mtu anayepinga Rushwa
ndani ya CCM watakwenda kumtafuta nje ya CCM.Swali kwa uchaguzi huu wa
mwaka 2015,Mtu anayepinga RUSHWA yupo ndani ya CCM au Nje ya CCM?? Jibu
ni yupo ndani ya CCM na yule mwenye sifa ya kula Rushwa na kuiba mali za
Umma yupo NJE ya CCM.Hivyo Watanzania wanatakiwa kuiingua Mkono CCM na
sio hao wengine.
Jambo la pili MUUNGANO, Mwl.Nyerere
alisema Kiongozi Mkubwa kama Rais ni lazima autetee Muungano wa Nchi
yetu.Hivyo Watanzania wasipopata Mgombea ndani ya CCM anayeweza kuutetea
Muungano wetu,Watakwenda NJE ya CCM kumtafuta mtu anayeweza kutetea
Muungano wetu. Swali,Kati ya CCM na Wagombea wengine ni Mgombea yupi
anasera za kuutetea Muungano wetu??Rejea kauli ya Mwl.Nyerere kuwa
serikali tatu(3) ni kuua Muungano wetu.
Jambo la tatu ni UDINI na UKABILA,Mwl.Nyerere
alisema ,Kiongozi wa Taifa kubwa kama Tanzania ni lazima adumishe
Ummoja kwa kuzuia Udini na Ukabila.Hivyo Watanzania wasipopata Mgombea
Urais anayeweza kukemea Udini na Ukabila bila kuuonea haya watakwenda
nje ya CCM kutafuta mtu anayekemea Udini na Ukabila.Swali,Kwa wagombea
wa sasa kwenye Uchaguzi huu 2015 ni Mgombea yupi anaeneza UDINI na
Ukabila na Yupi anakemea Udini na Ukabila??
Uchaguzi Mkuu wa wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania wa Rais , Wabunge na Madiwani unatarajiwa kufanyika
Oktoba mwaka hii nchini kote ukishirikisha vyamba mbalimbali vya
kisiasa.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-MUSOMA)
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli
akihutubia maelfu ya wananchi mjini Musoma katika mkutano uliofanyika
leo kwenye viwanja vya Mkendo.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli
akisisitiza jambo wakati akitoa hotuba yake mjini Tarime.
Mwigulu Nchemba akihutubia mkutano wa kampeni katika viwanja vya Mukendo mjini Musoma
Jaji Mstaafu Mzee Joseph Sinde
Warioba akizungumza na wananchi wa mjini Tarime wakati alipokuwa
akimpigia debe Dr. John Pombe Magufuli.
Umati wa wananchi waliohudhuria kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Tarime mkoani Mara.
Vijana hawa wakiwa wamejipaka rangi CCM za mwilini mwao kama ishara ya kukipenda chama hicho.
Umati wa wananchi wakiwa
wamejitokeza kwa wingi katika mkutano wa kampeni wa CCM uliofanyika
kwenye viwanja vya Mkendo mjini Musoma
Baadhi ya wazee wakipmokea Dr. John Pombe Magufuli alipowasili mjini Tarime mkoani Mara.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli
akipiga Drums Ngoma za muziki wakati alipofika Utegi wilaya ya Rolya na
kufanya mkutano wa kampeni.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli
akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika Utegi wilayani Rolya.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli
akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Rolya Mh.Okambo Lameck Airo mjini
Utegi.
Mgombea Ubunge wa jimbo la Rolya
Mh.Okambo Lameck Airo akiomba kura kwa wananchi wa Utegi huku Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr.
John Pombe Magufuli akimsikiliza katikati ni Mzee Jaji Joseph Warioba.
Makongoro Nyerere akimpigia debe Dr. John Pombe Magufuli katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Musoma.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli
akiongozana na Mgombea Ubunge wa jimbo la Musoma Vijijini Profesa
Sospeter Muhongo wakati alipowasili katika shule ya msingi Nyasurura.
Kikundi cha Ngoma kikitumbuiza katika kijiji cha Nyasurura.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli
akiteta jambo na Jaji Joseph Warioba katika kijiji cha Nyasurura
kushoto ni Makongoro Nyerere.
Kundi la TOT likifanya vitu vyake katika mkutano huo.
Mzee Steven Wasira kulia akizungumza na Mwigulu Nchemba.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli
akimsikiliza Mwigulu Nchema wakati alipokuwa akizungumza naye.
Kada wa CCM Amon Mpanju akizungumza na wananchi wa Musoma mjini wakati alipokuwa akimpigia debe Dr. John Pombe Magufuli.
Mzee Steven Wasira akihutubia mkutano wa kampeni katika viwanja vya Mukendo mjini Musoma.
Mzee Jaji Joseph Warioba
akiwahutubia wananchi wa Musoma katika mkutano wa kampeni uliofanyika
kwenye uwanja wa Mukendo mjini Musoma.
Mwigulu Nchema Kulia na Makongoro Nyerere akiwateta jambo wakati wa mkutano huo.
Ndugu Vedastus Mathayo mgombea
ubunge jimbo la Musoma mjini CCM akiwaomba kura wananchi katika mkutano
wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Mukendo.
Umati wa wananchi ukinyoosha
mikono yao juu kuashiria kumkubali Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano
ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli.
Uwanja wa Mukendo ukiwa umejaa wananchi.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli
akiondoka huku akiwapungia wananchi mkono mara baada ya kumaliza
kuhutubia mkutano huo uliofanyika uwanja wa Mukendo mjini Musoma.
Wananchi nao wakimpungia mikono kuashiria kumuaga.
Kwa heri Musoma.
No comments:
Post a Comment