Saturday, September 12, 2015

Tanzania yashika nafasi ya pili katika malipo kupitia simu za mkononirevolution
Kumiliki simu ya mkononi imekuwa si jambo la starehe kama miaka ya nyuma ilivyokuwa inasadikika. Kadri miaka inavyozidi kwenda kumekuwa na matoleo mapya ya simu za mkononi na huduma za kipekee zilizo na manufaa kwa jamii.
Meneja mkazi wa JovagoTanzania, Bw.Andrea Guzzoni amefafanua kwamba “kadri matumizi ya simu za kisasa yanavyoongezeka, kunakuwa na huduma tofauti za malipo kupitia simu za mkononi (Online payments), malipo haya yameongezeka kwa kasi kubwa kupitia Mpesa, Tigopesa, Airtel money na malipo ya kibenki (simu banking) ambapo Kenya imeshika nafasi ya kwanza ikifuatiwa naTanzania katika nafasi ya pili kwa 53% ya huduma hizo za malipo
Kwa Upande wake Afisa meneja mawasiliano wa JovagoTanzania, Lilian Kisasa aliongeza kwa kusema kuwa, pamoja na ongezeko la matumizi ya simu za kisasa, bado kuna asilimia chache ya watu wanaoweza kutembelea tovuti mbali mbali kwa lengo la kujifunza na kutafuta huduma za kenye mitandao, hivyo bado tunahitaji kujiamini katika kutumia huduma za mitandaoni kwani kuna baadhi ya tovuti hazina utapeli na zina faida kwa jamii.
Hata hivyo, soko hili la simu linabadirika kila baada ya mwezi, mwaka au miaka miwili, kwa kipindi cha nyuma kulikuwa na matolea ya zamani ambazo simu nyingi zilikuwa na uwezo mdogo wa internet na kumfanya Mtanzania kupata wakati mgumu iwapo atahitaji huduma yeyote ya mtandaoni. Lakini kwa hivi sasa kumekuwa na tano bora ya simu za kisasa ambazo zinanunuliwa kwa kasi ambazo ni Samsung, Nokia, na Iphone, simu hivi ni chachu ya maendeleo katika jamii, “bado tuanaamini hivyo kwa kuwa zinauwezo mkubwa wa kutoa huduma yoyote kupitia playstore au ios kutegemea na hitaji la mtumiaji” alifafanua.
Hata hivyo, kutokana na takwimu zilizofanywa na jovagoTanzania, Kampuni inayojihusiha na soko la mtandaoni, inaonyesha kuwa kumekuwa na ongezeko la 15% katika nchi za Afrika ya mashariki na kukadiriwa kutakuwa na ongezeko la zaidi ya 33% katika miaka mitatu ijayo. Kwa sababu hiyo, bado kuna nafasi kubwa ya watanzania kunufaika na ulimwengu huu wa kidigitali kwa kupata huduma tofauti za mitandaoni zitakazoendelea kujitokeza kila mwaka , mfano kwa sasa mtanzania anauwezo wa kuagiza chakula kupitia Hellofood, kununua mavazi au bidhaa za ndani kupitia Kaymu na kubook vyumba vya hotelini kutoka Jovago.com kwa simu zao mkononi.
Post a Comment