Ndugu zangu,
Fredrick Tluway Sumaye ni mmoja wa walioshindwa sana kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Ni heri
ya Lowassa na Kingunge kulikoni Sumaye. Nilibaki nikimshangaa Sumaye
aliposimama majukwaani na kuiponda CCM huku akilaumu pia Katiba
inayovikandamiza vyama pinzani.
Katika
uchaguzi wa mwaka huu yumkini wapiga kura wamewaadhibu watu wa aina ya
Sumaye na kuwaonyesha, kuwa wao wapiga kura si wajinga.
Nilimshangaa
Sumaye na Kingunge kusimama majukwaani na kulaumu mfumo ambao wao
walishiriki kuujenga na kuulinda. Kwa Sumaye na Kingunge wanapolaumu
Tume ya Uchaguzi na Katiba ya Nchi ya mwaka 1977 wanasahau, kuwa wao
wakiwa madarakani walikuwa na nafasi ya kuweka mazingira ya kufanyiwa
mabadiliko.
Ona
Fredrick Sumaye, ukiacha mapendekezo ya Jaji Francis Nyalali ya mwaka
1992 ambayo yaliainisha sheria 40 kandamizi, na hata Sumaye alipoteuliwa
kuwa Waziri Mkuu mwaka 1995, sheria hizo 40 kandamizi alizikuta,
hakufanya lolote.
Mwaka
1998, Ben Mkapa aliunda Tume ya Jaji Kissanga iliyomkuta Sumaye akiwa
Waziri Mkuu. White Paper ile ya Jaji Kissanga, mbali ya mambo mengine,
ilipendekea pia Rais achaguliwe kwa kupata 50 plus asilimia za kura
zote. Ikapendekeza pia Serikali tatu katika muundo wa Muungano.
Nakumbuka pale Diamond Jubilee Hall, Ben Mkapa akiongea na wazee wa
darisalaam aliinanga ripoti ya Jaji Kissanga akidai pia haikufuata adidu
za rejea. Sumaye alikuwepo kama Waziri Mkuu, alikuwa na nafasi ya
kuweka mazingira ya kurekebishwa kwa sheria hizo, lakini, wakati huo,
alikaa kimya.
Sumaye alikuwa bize akichimba kisima ambacho leo ameingia mwenyewe.
Niwe
mkweli kwa nchi yangu, Fredrick Sumaye wa leo, kama alitaka mabadiliko
ya kweli, alipaswa kuendelea kubaki CCM na kuifanya kazi hiyo ndani ya
CCM- kama ' Born Again Sumaye' . Angelikuwa na jukwaa pana zaidi na
angeaminika zaidi.
Ni dhahiri, kuwa matokeo ya uchaguzi mkuu yamemtumbikiza Fredrick Sumaye kwenye kisima alichokichimba mwenyewe. Inasikitisha.
Ni mtazamo wangu.
Maggid,0754 678 252
Iringa
No comments:
Post a Comment